Habari za Punde

ZECO Yakabidhi Hundi ya Shilingi Milioni Hamsini

Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar {ZECO} Nd. Hassan Ali amkimkabidhi Hundi ya Shilingi Milioni 50,000,000/- Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho ya Kitaifa Balozi Seif Ali Iddi kusaidia maandalizi ya Shere za Mapinduzi kutumia Miaka 56.
Balozi Seif  Kulia akipokea Fulana na Kafia zake 300 kutoka kwa Uongozi wa Shirika la Umeme Zanzibar {ZECO} zitakazotumika katika Sherehe za Mapinduzi kutimia Miaka 56.
Balozi Seif Ali Iddi Kati kati akiupongeza Uongozi wa Shirika la Umeme Zanzibar kwa moyo wa Kizalendo kuchangia Maandalizi ya Sherehe za Mapinduzi Mwaka 2020.
Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar Nd. Hassan Ali akizungumza katika hafla ya kukabidhi mchango wa Shilingi Milioni 50,000,000/- kusaidia maandalizi ya Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.


Uongozi wa Shirika la Umeme Zanzibar {ZECO} Umekabidhi mchango wa Shilingi Milioni 50,000,000/- Taslim pamoja na Fulana na Kofia zake 300 kwa ajili ya kusaidia maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Mapunduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia Miaka 56 zinazoanza Rasmi kila ifikapo Tarehe 31 Disemba kwa usafi wa mazingira.
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar Nd. Hassan Ali akiiongoza Timu ya Viongozi Wanne wa Shirika hilo alikabidhi hundi ya Fedha hizo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimidho ya Kitaifa ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.
Ndugu Hassan Ali alisema Uongozi wa Shirika hilo umefikia hatua hiyo katika azma ya kuendelea kuthamini na kuenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 yaliyowakomboa Wakwezi na Wakulima wa Visiwa vya Unguja na Pemba kutoka katika makucha ya Wakoloni.
Alisema licha ya udogo wa Mchango huo lakini alieleza kwamba unaweza kuongeza nguvu na kasi katika matayarisho ya sherehe hizo zilizozunguukwa na mambo mengi yanayohitaji kuungwa mkono na kila Mwanamapinduzi wa Taifa hili.
Akipokea mchango huo Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliushukuru Uongozi wa Shirika la Umeme Zanzibar {ZECO} kwa moyo wa kizalendo uliyoonyesha wa kuthamini tukio hilo la Kihistoria.
Balozi Seif alisema katika mazingira ya kawaida ya Wanaadamu hakuna msaada mdogo unaotolewa miongoni mwao lakini kinachohitajika ni kwa wale wanaopewa msaada husika kujenga matumaini ya kuithamini hidaya hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwakumbusha Watendaji wa Shirika la Umeme Zanzibar kugharamika katika ujenzi wa miundombinu ya Umeme itakayowawezesha kuongeza wateja zaidi ambao watakuwa wakichangia Mapato ya shirika hilo kwa ununuzi wa huduma ya Umeme kila wakati.
“ Mnapoona Nyumba Mpya inajengwa katika eneo lolote lile hapa Nchini ni vizuri mkaanza kampeni ya kumpata mmiliki wake kwa kumtayarishia mazingira rafiki ya kumpatia huduma hiyo”. Alisema Balozi Seif.
Alisema ujenzi wa Nyumba Mpya na za kisasa zinazohitaji Huduma za Umeme katika maeneo mbali mbali Nchini hivi sasa imezidi kupamba moto jambo ambalo ZECO wanaweza kuitumia fursa hiyo katika kuongeza Wateja wapya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.