Habari za Punde

Uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi na Salama Kijiji Cha Mtangani Wilaya ya Mkoani Pemba.

Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Moh'd, akizinduwa mradi wa Maji Safi na Salama huko Mtangani Mkoani Pemba, uliofadhiliwa na Serikiali ya watu wa China.
Ofisa Maji Wilaya ya Mkoani Pemba, Mohammed Mbarawa Mnyaa, akifunguwa mashine ya maji kwenye mradi uliofadhiliwa na Serikali ya watu wa China huko katika kijiji cha Mtangani Wilaya ya Mkoani Pemba ili kuonesha mafanikio yake.


Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid Mohammed, akiwahutubia Wananchi na Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama , uliofadhiliwa na Serikali ya watu wa China huko Mtangani Pemba.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya watu wa China, wakiwa katika uzinduzi wa mradi wa Maji Safi na Salama , huko katika Kijiji cha Mtangani Wilaya ya Mkoani Pemba, uliofadhiliwa na Serikali ya watu wa China.
Baadhi ya Wananchi wa waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama uliofadhiliwa na Serikali ya watu wa China huko Mtangani Mkoani Pemba.
Baadhi ya Wananchi wa waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama uliofadhiliwa na Serikali ya watu wa China huko Mtangani Mkoani Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.