Naibu Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa Na Michezo Juliana Shonza akipokea tuzo kwa niaba ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Desemba 5,
2019 katika ukumbi wa Karimjee uliopo jijini Dar es salaam aliyotunukiwa na
Shirika lisilo la Kiserikali la Kuinua Diplomasia ya Uchumi Tanzania (TEDEF)
kwa kuwa mstari wa mbele kuinua diplomasia ya uchumi nchini.
Na Eleuteri Mangi,
WHUSM, Dar es Salaam
Shirika lisilo la Kiserikali
la Kuinua Diplomasia ya Uchumi Tanzania (TEDEF) limetambua juhudi na kuthamini
kazi anazofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. John Pombe
Magufuli kuhakikisha azma ya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025
inafikiwa.
TEDEF imemtunuku tuzo
Rais Dkt. Magufuli na kuwa miongoni mwa
Watanzania 10 waliofanya vizuri kwa kutoa mchango wao katika kuimarisha
Diplomasia ya Uchumi wa nchini.
Akipokea tuzo hiyo
kwa niaba ya Rais Dkt. Magufuli na kuwakabidhi tuzo hizo watanzania wengine waliomstari
wa mbele kuinua diplomasia ya uchumi nchini Desemba 5, 2019 katika ukumbi wa
Karimjee uliopo jijini Dar es salaam, Naibu Waziri Wa Habari, Utamaduni, Sanaa
Na Michezo Juliana Shonza ameishukuru TEDEF kwa uamuzi wao wa kushirikiana
na Serikali katika kuimarisha diplomasia ya Uchumi
nchini.
“Diplomasia
ya Uchumi ni
Muhimu kwa ustawi
wa Taifa. Mataifa yote makubwa duniani yameupa umuhimu
wa kwanza Diplomasia ya Uchumi ambao umekuwa ni muhimili wa kukuza mataifa
hayo. Nanyi TEDEF mmekuwa wazalendo kwa kutambua na kuthamini mchango wa
viongozi na wananchi mbalimbali katika kuhakikisha nchi yetu inafikia azma yake
ya kuwa nchi ya uchumi wa kati” alisema Naibu Waziri Shonza.
Miongoni mwa kazi zilizomfanya
Rais Dkt. Magufuli kupewa tuzo hiyo mchango wake katika kujenga miundombinu ya
kufanikisha Diplomasia ya Uchumi
Tanzania ikiwemo miradi ya reli ya kisasa (SGR), kuimarisha shirika la ndege, ujenzi wa barabara na madaraja
mbalimbali nchini pamoja na Mradi
wa umeme Bwawa la Nyerere.
Watanzania wengine waliopata
tuzo za kushiriki kujenga diplomasia ya uchumi ni mawaziri wawili ambao ni
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba
Kabudi kwa kuongoza majadiliano ya
Biashara ya Kimataifa baina ya Tanzania
na Kampuni ya Madini
ya Barrick kwa mafanikio makubwa kwa Tanzania pamoja na Wiziri wa Mambo
ya Ndani nchi Kangi Lugora ambaye anasimamia
ulinzi na usalama wa raia na mali zao kwa kutambua amani iliyojengeka ni muhimu
kwa kufanikisha Diplomasia ya Biashara na Diplomasia ya Uchumi.
Tuzo hizo pia
zimeenda kwa Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi ambao nao
wametambuliwa kwa mchano wao katika kujenga diplomasia ya uchumi; Ubalozi wa
Tanzania Nchini Rwanda ukiongozwa na Balozi Ernest Mangu ambao umeongoza kwa
mauzo ya nje katika nchi za Afrika Mashariki, Ubalozi wa Tanzania nchini China
ukiongozwa na Balozi Mbelwa Kairuki kwa kwa kuongoza katika uwekezaji mitaji
nchini pamoja na Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani ukiongozwa na Balozi
Wilson Masilingi ambao umeongoza kwa kuleta watalii nchini.
Mbali na viongozi
hao, Mkoa wa Dar es Salaam ambao unaongozwa na Mkuu wa mkoa huo Paul Makonda nao
umepata tuzo hiyo kwa kuongoza kwa miradi
ya uwekezaji ambapo takribani miradi 109 imesajiliwa.
Aidha, Watanzania
wengine ambao wametambuliwa kwa mchango wao katika kushiriki katika kuitangaza
Tanzania kimataifa katika diplomasia ya uchumi na kupewa tuzo hiyo ni mchezaji
wa mpira wa miguu Mbwana Samata kupitia sekta ya michezo, mwanamuziki Nasibu
Abdul (Diamond) kupitia sekta ya muziki pamoja na mtangazaji wa TBC Elisha Elia
anayetangaza kipindi cha Kishindo cha Awamu ya Tano na
kusaidia kutangaza miundombinu ya
Diplomasia ya Biashara na Diplomasia ya Uchumi kupitia sekta ya habari.
Kwa upande wake
Mkurugenzi na Makamu Mwenyekiti Bodi ya TADEF Dkt. Wilbroad Mtabuzi ameyataja baadhi
ya majukumu ya msingi ya shirika hilo kuwa ni pamoja na kuvutia
uwekezaji hasa kwenye viwanda, Kuhamasisha biashara ya kimataifa kuhamasisha utalii,
kutangaza sifa njema za nchi yetu ambayo
ni amani, utulivu na umoja wa Kitaifa
ambapo majukumu hayo yatasaidia kuchangia kasi yakuufikia uchumi wa kati.
Dkt. Mutabuzi amesema
kuwa TEDEF imefanikiwa kuunda vyama vya ushirika kwa wahimitimu wa elimu ya juu
nchini ambao wamejiajiri katika katika sekta ya kilimo-biashara kwenye
mikoa ya mikoa
ya Dare es
salaam, Pwani, Dodoma, Kigoma,
Mbeya na Mwanza.
Wahitimu hao
wamefanikiwa kuanzisha vikundi vya ufugaji samaki kibiashara katika mkoa wa
Pwani eneo la Ruvu wilayani Bagamoyo pamoja na kuwasaidia wakulima zaidi ya
2000 wanaojishughulisha na kilimo wamenufaika na huduma za TEDEF nchini.
Sera ya Diplomasia ya
Uchumi Mwaka 2001 nchini ilianza kutekeleza kufuatia idhini ya Rais wa Awamu ya
Tatu Benjamin William Mkapa mwaka 2000 ikitambua kuwa Diplomasia ya Uchumi ni
Ustawi ambapo ushiriki wa TEDEF katika diplomasia hiyo una mchango katika
kuleta ustawi katika nchini.
No comments:
Post a Comment