Na.
Immaculate Makilika – MAELEZO
Mauzo ya bidhaa nje ya
nchi zisizo kuwa za kawaida yameongezeka kwa asilimia 41.9 kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), mwezi Novemba, mwaka jana.
Hayo yamesemwa leo Jijini
Dodoma na Mkurugenzi wa Idara ya Habari
- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi alipokuwa akizungumza
na waandishi wa habari .
Dkt. Abbasi amesema kuwa
kupitia jitihada mbalimbali zinazochagizwa na Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John
Pombe Magufuli zimesaidia kuongeza ukusanyaji wa mapato, kuongeza mauzo ya
bidhaa muhimu kwenda nje na ukuaji wa viwanda nchini ikiwa ni sehemu muhimu ya mageuzi ya uchumi nchini.
“Wote mnafahamu kuwa
Serikali imechukua hatua kubwa kuanzisha masoko ya madini na kuzuia uuzaji
holela na utoroshaji wa madini. Matokeo yake tumeanza kufaidi. Hadi Novemba,
2019, mauzo ya dhahabu nje ambayo ni asilimia 51.4 ya mauzo yote ya bidhaa nje
ya nchi yaani bidhaa zisizo za kawaida, yaliongezeka kwa asilimia 41.9 kufikia
kiasi cha Dola Bilioni 2.1”, alisema Dkt. Abbasi
Aidha, aliongeza kuwa “sera ya kuchagiza
ujenzi wa viwanda nayo imezidi kulipa, ambapo
mauzo ya bidhaa za viwandani nje ya nchi
yameongezeka kwa asilimia 28.4 kufikia Dola milioni 996.0 ikichangiwa
zaidi na bidhaa za chuma na mabati, vioo, tumbaku, katani na mbolea.
Jitihada hizo za
Serikali zimeendelea kusaidia kuongeza ajira kwa watanzania, sambamba na kuwa
vyanzo vipya vya mapato huku vikitazamiwa kusaida uboreshaji wa huduma za
kijamii.
No comments:
Post a Comment