Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATUI YA SIASA MKOA WA DAR NA PWANI

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar xes salaam Bibi Katwe Kamba alipowasili  katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Dar es salaam Lumumba leo Januari 30,2020 kwa ajili ya kuongoza  kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dar es salaam kilichojadili namna ya kuadhimisha miaka 43 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na utatuzi wa baadhi ya Changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu ya Chama pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi mwaka 2015, 2020.  

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dar es salaam kilichokutana leo Januari 30,2020 katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Dar es salaam Lumumba kwa ajili ya kujadili namna ya kuadhimisha miaka 43 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na utatuzi wa baadhi ya Changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu ya Chama pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi mwaka 2015, 2020.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.