Naibu Waziri Wizara
ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (aliyeketi watatu kushoto) akitizama filamu
ya masanii wa filamu Maria Luya aliyomkabidhi wakati alipokuwa akifanya kikao na wadau wa tansia ya filamu mkoa wa
singida hawapo pichani,wa kwanza kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu
Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo, na wapili kushoto ni Katibu Tawala Wilaya ya
Singida Wilson Shimo.
Na Anitha Jonas –
WHUSM. -Singida.
Naibu Waziri Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe.Juliana Shonza amewasisitiza wanatasnia ya filamu kuhakikisha wanarasimisha
kazi zao na kujisajili.
Mheshimiwa Shonza
ametoa agizo hiyo leo
Mkoani Singida alipokuwa akifanya kikao na wadau wa
tasnia ya filamu wa mkoa huo kwa lengo la kutaka kusikiliza kero zao na
kuwaeleza wadau hao mikakati ya serikali katika kuboresha tasnia hiyo,kuthibiti
uharamia ili kuhakikisha wanafaidika na
kazi zao.
Akiendelea kuzungumza
katika kikao hicho Naibu Waziri huyo aliwasisitiza wanatasnia hao wa filamu kuzingatia
suala la uandaaji wa muswada wa filamu na kupeleka miswada hiyo kwa maafisa
utamaduni kwa ajili ya ukaguzi na kupata
ushauri wa filamu watakayoandaa sababu
hiyo ni moja ya njia itakayosaidia kuandaa kazi zenye ubora.
“Kwanza ningependa
niwashauri muache kusambaza au kuuza kazi zenu kwa njia ya ‘flash’ katika
vibanda vya kuuza filamu sababu hii bado ni njia inayowakandamiza na hauwezi
kupata faida ya kazi yako, sasa hivi kazi hizo za filamu zinasambazwa kwa mfumo
wa kidigitali mfano kwenye Swahilifilx na Netflix,kikubwa ni kazi yako iwe
yenye ubora na iliyozingatia utaratibu wa kitaalamu katika kuandaa filamu
ikiwemo wachezaji kuvaa uhusika na
kucheza katika maeneo yenye uhalisia wa filamu hiyo,”alisema Mhe.Shonza.
Naye Kaimu Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo bodi imekuwa ikitoa mafunzo kwa wadau wa tasnia
hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuandaa kazi bora zitakazo kuwa na
ushindani kwa ndani na nje ya nchi na kwa hivi karibuni wanatarajia kufanya
mafunzo hayo mkoani Dodoma na kwa wadau wa Singida ambao hawajawahi kupata
mafunzo hayo wanakaribishwa kushiriki.
“Bodi ya filamu
katika kuimarisha masoko ya usambazaji wa filamu ndani na nje ya nchi imempata
mdau kutoka Nigeria mwenye Kampuni iitwayo
ENVIVO ambaye yupo tayari kununua jumla
kazi mia moja mpaka ifikapo mwezi Juni mwaka huu,zenye hadithi mbalimbali za
kitanzania ambapo zitatafsiriwa kwa lugha kwa lugha ya Yoruba,Pijini na Igbo kusambazwa,kikubwa katika kazi hizo
ni ziwe zimebeba hadithi za kitanzania na zenye ubora na pia ziwezinaendana
na muswada,”alisema Dkt.Kilonzo.
Pamoja na hayo
Dkt.Kilonzo aliwasihii wadau hao kuwa mfumo wa usambazajiwa kwa kazi za filamu
kwa sasa umebadilika na filamu kwa sasa mara baada ya kukamilika inafanyiwa
uzinduzi katika majumba ya sinema na huko itaonyeshwa kwa kipindi fulani na
baadae inapelekwa katika mifumo mingine ya kidigitali na hatua ya kuiweka
katika CD na Youtube niyamwisho hii ni katika kulinda kazi hizo na uharamia pia
kuhakikisha msanii anapata faida ya kazi yake.
Kwa upande wa Afisa
Utamaduni Mkoa Bw.Hendry Kapera alisema wasanii wengi wa filamu katika mkoa huo
hawataki kujisajili wala kurasimisha kazi zao hii ni changamoto kubwa na
wamekuwa wakijiweka mbali na maafisa utamaduni wa wakihofia kuulizwa kuhusu
usajili na hii imechangia wao kuandaa kazi zisizo na ubora sababu hawapendi
kushirikiana na maafisa hao.
Halikadhilika nae
mmoja ya wasanii hao wa filamu kutoka Wilaya ya Ikungi Bw.Salumu Ntandu aliomba bodi ya filamu
kuwapatia mafunzo wadau hao wa mkoa huo na pia aliwasihii wasanii wenzake kuwa
na umoja na kuacha migogoro kwani umoja wao ndiyo utakaoweza kutangaza kazi zao
na kutangaza mkoa wao pale watakapo andaa kazi nzuri zenye ubora na
kushirikishana katika kuitangaza na kuizindua.
Naibu Waziri Wizara
ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akizungumza na wadau wa tasnia ya filamu Mkoa
wa Singida leo na kuwasisitiza kurasimisha kazi zao pamoja na
kujisajili,katika kikao cha kusikiliza
kero za wadau hao na kuwaeleza mikakati ya serikali katika kuimarisha tasnia hiyo kilichoandaliwa na Bodi ya Filamu
Tanzania.
Kaimu Katibu Mtendaji
Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo akizungumza na wadau wa tasnia ya
Filamu Mkoa wa Singida leo kuhusu mikakati ya bodi ya filamu katika kuimarisha
mazingira ya usambazaji wa kazi za filamu nje ya nchi ambapo wameipata kampuni
kutoka Nigerea itakayo nunua filamu mia moja zenye hadithi za asili ya
kitanzania,wapili kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe.Juliana Shonza ,wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala Wilaya ya
Singida Wilson Shimo na wa kwanza
kuliani Afisa Utamaduni Mkoa wa Sngida
Bw.Hendry Kapera.
Msanii wa Komedi
kutoka kikundi cha Magic Sanaa Group Singida Mjini kutoka Kata ya Mwenge Bw.Yusuph Ally akitoa maombi yake kwa uongozi wa bodi ya filamu kuwapatia vitambulisho wasanii
wa mkoa huo leo katika kikao cha Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe.Juliana Shonza na
viongozi wa bodi ya Filamu hawapo pichani.
Naibu Waziri Wizara
ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (aliyeketi wapili kushoto) akimsikiliza Msanii wa Filamu Mkoa wa Singida
Bi.Maria Luya akimweleza stori ya kuhusu
filamu yake iitwayo furaha kabla ya kumkadhi leo katika kikao chake na wadau
hao wa filamu kilichofanyika Mkoani Singida,wa kwanza kulia ni Katibu Tawala Wilaya
ya Singida Wilson Shimo na wa pili kulia ni Kaimu ni Katibu Mtendaji Bodi ya
Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza aliyeketi watatu kushoto akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa tasnia ya filamu Mkoani Singida leo mara baaada ya kulamizika kikao cha kusikiliza kero za wadau hao na kueleza mipango ya serikali katika kuimarisha sekta hiyo na kuthibibiti uharamia wa kazi za filamu na kuhakikisha msanii ananufaika na kazi yake,wa pili kulia Kaimu ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo pamoja na Katibu Tawala Wilaya ya Singida Wilson Shimo.
No comments:
Post a Comment