RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,
akimtunuku Nishani ya Mapinduzi kwa Viongozi na Wananchi Wenye Sifa Maalum,Ndg.Zaidi
Juma Ussi, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.ikiwa
ni shamrashamra za kuadhiumisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ametunuku
Nishani ya Mapinduzi, Nishani ya Utumishi Uliotukuka pamoja na Nishani ya
Ushujaa kwa Viongozi, Watumishi wa
Umma, Maafisa na Wapiganaji wa Idara Maalum za SMZ na wananchi mbali mbali wenye sifa maalum.
Hafla hiyo ilifanyika
katika viwanja vya Ikulu jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali
wa Serikali, Vyama vya siasa, viongozi wakuu wastaafu akiwemo Rais Mstaafu wa Awamu
ya Sita wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume, Makamo wa
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Kharib Bilal.
Viongozi wengine
waliohudhuria ni Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika
wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman
Makungu, Waziri Kiongozi Mstaafu Shamsi Vuai Nahodha, Mawaziri na viongozi
wengine wa Serikali, wananchi na wanafamilia, hafla ambayo ni muendelelezo wa
shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964.
Mapema akitoa tamko la Kwanza la kuashiria kuanza
shughuli hiyo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Salum Maulid Salum alisema kuwa Rais Dk. Shein ametunuku Nishani 37 ya
Mapinduzi, Nishani 10 ya Utumishi Uliotukuka na Nishani 25 ya Ushujaa kwa
Viongozi, Watumishi wa Umma, Maafisa na Wapiganaji wa Idara Maalum za SMZ pamoja
na wananchi mbali mbali.
Katibu Mkuu huyo alieleza kuwa sherehe hiyo
ilihudhuriwa na watunukiwa 72 ambao kati ya hao 22 ni Marehemu ambao Nishani
zao zimepokelewa na wawakilishi wao na 50 wako hai ambapo nishani zao watapokea
wenyewe au zitapokewa kwa niaba yao.
Alisema kuwa Watunuku wote sifa zao zimekidhi
matakwa ya Nishani hizo ambapo Nishani ya Mapinduzi hutolewa kwa mtu ambaye
aliasisi au alishiriki au aliyatukuza na aliyaenzi Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari
12, 1964.
Aliongeza kuwa Mtunukiwa ni pamoja na Kiongozi au
mtu mwengine aliyehai au aliyefariki ambaye aliiletea sifa Zanzibar katika fani
mbali mbali na kuonesha maadili mema ya kusifika na kuigwa ambapo katika
Sherehe hizo, Nishani ya Mapinduzi inatunukiwa katika kundi la Viongozi na Wananchi
wenye sifa maalum.
Kwa maelezo ya Katibu Mkuu huyo Nishani ya Utumishi
uliotukuka hutolewa kwa Mtumishi wa Umma au Idara Maalum za SMZ aliyehai au
aliyefariki ambaye ametimiza Utumishi wake kwa muda wa miaka isiyopungua 20
mfululizo na kwa Mtumishi wa Idara Maalum za SMZ miaka isiyopungua 20 ya kuwa
Ofisa na katika kipindi chote hicho amekuwa na tabia njema.
Aliongeza kuwa Mtumishi huyo awe ametumikia Taifa
kwa Uzalendo wa hali ya juu na kufanya kazi kwa kujitolea, uwajibikaji,
uadilifu, ujasiri na umakini katika kusimamia majukumu na utendaji kazi.
Aidha, Katibu Salum alieleza kuwa Nishani ya
Ushujaa inatolewa kwa Mtumishi wa Idara Maalum za SMZ au mtu mwengine yoyote
aliyehai au aliyefariki ambaye ametenda kitendo cha Ushujaa, Ujasiri na
Uzalendo ambacho kimesaidia kuokoa mali au uhai wa mtu au kujitolea maisha yake
kwa ajili ya ulinzi wa Taifa.
Pamoja na hayo, Katibu Mkuu huyo alieleza kuwa
Vitendo hivyo vya ushujaa viwe wazi ambavyo mtunukiwa alivifanya na
kuthibitishwa, mahala popote pale penye hatari na ameendelea kuwa muaminifu na
mtiifu kwa nchi na Serikali yake.
Katika hafla hiyo, Dk.
Shein alitoa Nishani ya Mapinduzi kwa Viongozi na wananchi wenye sifa husika akiwemo
Asha Abdalla Juma, Meja Jenerali Mstaafu Khamis Rajab Semfuko, Kamishna wa Polisi
Mstaafu Marehemu Mussa Khamis Ramadhan, Kanal Mstaafu Ahui Hassan Ahui, Kapteni
Mstaafu Mohammed Mahamoud Juma, Kamanda Mstaafu Abdi Makame Mbai, Msaidizi
Mwandamizi Kamishna wa Polisi Mstaafu Saada Ibrahim Makungu.
Wengine ni Msaidizi
Kamishna wa Polisi Mstaafu Marehemu Issa Haji Pandu, Luteni Kamanda Mstaafu Ali
Yussuf Mohamed, Luteni Kamanda Mstaafu Shafi Mohamed Hanif, Kapteni Mstaafu
Marehemu Hassan Juma Reli, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Mstaafu Sofia Hebber Masewa
na Khatib Mwinyichande.
Rais Dk. Shein pia,
amewatunuku Profesa Ali Seif Ali
Mshimba, Amour Abdalla Khamis, Said Salim Bakhresa, Ahmada Yahya Abdulwakil,
Haji Mbarouk Ameir, Haji Nasibu Haji Nyanya, Khalid Ali Kombo, Khatib Haji
Khalid, Hassan Juma Khamis, Simai Jafar Bai, Zaidu Juma Ussi, Salmin Juma
Jecha, Haji Seti Haji.
Wengine waliotunukiwa
Nishani hizo ni Lela Nassor Khamis, Songoro Omar Kirobo, Khadija Hassan
Aboud, Fatuma Issa Juma, Daud Suleiman Ali, Marehemu Kheir Idd Milao, Marehemu
Ahmada Ali Shamata, Marehemu Hassan Juma Hassan, Marehemu Khamis Haji Mpera,
Marehemu Ame Vuaa Ame na Marehemu Abdi Ramadhan Shemhaji.
Rais Dk. Shein pia, ametoa
Nishani ya Utumishi Uliotukuka kwa Watumishi wa Serikali, Mahkama na Baraza la
Wawakilishi wakiwemo Maryam Abdallah Yussuf, Zuleikha Kombo Khamis, Janeth Nora Sekihola,
Saleh Ali Salim, Luteni Kamanda Subira Mohamed Hassan, Marehemu Juma Ali Juma,
Marehemu Silima Mkindwi Khamis, Marehemu Abdallah Waziri Ramadhan, Marehemu
Balozi Ali Othman Korosheni na Marehemu Abel Anthony De Silva.
Sambamba na hayo, Rais
Dk. Shein ametunuku Nishani ya Ushujaa kwa Watumishi wa Idara Maalum za
SMZ akiwemo Luteni Kanali Mstaafu Ali
Ussi Ali, Luteni Kanali Mstaafu Justice Issack Anthony, Meja Mstaafu Mohamed
Hamza Yussuf, Kapteni Mstaafu Fatma Abdalla Mussa, Kapteni Mstaafu Juma Ali
Jongo, Kapteni Mstaafu Ramadhan Mango Jilungui, Luteni Mstaafu Abdalla Hassan
Rehani, Waranti Ofisa Mteule Daraja la I Mstaafu Kona Haji Juma, Ofisa Mteule
Daraja la 2 Mstaafu Othman Bakari Kwae.
Wengine ni Ofisa Mteule
Daraja la 2 Mstaafu Abdallah Ali Abdallah, Sajin Taji Mstaafu Suleiman Mgeni
Suleiman, Sajin Taji Mstaafu Rehani Uled Khamis, Sajin Mstaafu Iddi Khamis
Omar, Sajin Mstaafu Ali Khatib Ali, Koplo Mstaafu Ali Haji Issa, Sea 1. Ali
Mossi Haji na Hija Hassan Hija.
Pamoja na hao, Rais
Dk. Shein pia, alimtunuku Koplo Marehemu Said Abdulrahman Juma, Private
Marehemu Sharif Salim Suleiman, Police Constable Marehemu Haji Muslim Simai, Mrehemu
Bakari Juma Hussein, Marehemu Ali Juma Ame, Marehemu Hafidh Silima Kona,
Marehemu Issa Daud Omar na Marehemu Mohamed Abdallah Mohamed.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment