
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na
Mazingira Mhe. George Simbachawene
akikagua sakafu ya jengo la machinjio katika eneo la Msalato jiijini
Dodoma wakati wa ziara ya kutembelea machinjio hiyo. Wengine katika picha hiyo
ni Afisa Mipango miji jiji la Dodoma Bwana Shabani Juma na Mwenyekiti wa Bodi
ya NEMC Profesa Esnath Chaggu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na
Mazingira Mh. George Simbachawene
akiongea na Diwani wa Kata ya Msalato Mh. Ally Mohamed wakati wa ziara hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene hii leo amegoma
kufungua machinjio ya Msalato jijini Dodoma kwa kutokidhi vigezo vya ubora vinavyoridhisha
ikiwemo ukarabati wa kiwango cha chini na kutoa muda wa wiki ya moja
kurekebisha dosari zilizobainika.
Ametoa uamuzi huo wakati
akitembelea jengo la machinjio ya Msalato jijini Dodoma wakati wa ziara
aliyoifanya na kubaini kasoro mbalimbali zinazotakiwa kupatiwa ufumbuzi.
“Sifungui hii machinjio kwa sababu hamjajiandaa na ujenzi uko hovyo kwahiyo
siwezi kufungua kitu cha hovyo namna hii” Simbachawene alisisitiza.
Akiongea katika ziara hiyo
amesema amesikitishwa sana na ukarabati wa kurekebisha machinjio hayo kwani haukidhi
viwango na ujenzi wake ni wa kiwango cha chini hivyo amemuagiza Afisa Mipango
Miji wa Jiji la Dodoma Bwana Shabani Juma kuhakikisha ndani ya wiki ya moja
kila kitu alichotolea maelekezo kifanyiwe marekebisho.
“Sijafurahishwa kwa kwakweli,
majengo ya Serikali yanatakiwa kujengwa na mafundi classic, vitu vya Serikali viwe State
of Art” Simbachawene alisisitiza.
Waziri Simbachene pia
amegiza kuandaliwa kwa taarifa rasmi ya ukarabati huo ikiwa ni pamoja na
thamani ya fedha zilizotumika katika zoezi zima la ukarabati na ujenzi wa mifumo ya maji safi na maji taka.
Naye Diwani wa Kata ya
Msalato Mheshimwa. Ali Mohamed amesema kuwa amesikitishwa sana kwa kutofunguliwa
kwa machinjio hiyo kwani wakazi wengi wa Kata yake wanategemea machinjio kwa
shughuli zao za kila siku kwa sababu ni Wafugaji. Pia alisema Maelekezo yote
yaliyotolewa na Mheshiwa Waziri Simbachawene wameyapokea na naamini kuwa
yatarekebishwa kwa wakati.
Machinjio hiyo ya Msalato
ilifungwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimazi wa Mazingira (NEMC) tarehe 31
Oktoba 2019 kutokana na sababu za mazingira yasiyokua safi na salama, kufuatia
ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira.
No comments:
Post a Comment