Habari za Punde

Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Amani Zanzibar Wakabidhi Vifaa Kwa Ajili ya Shehia za Jimbo la Amani Wakitimiza Ahadi Zao Kwa Wananchi

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe.Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Vifaa vya Ujenzi kwa Ajili ya Jimbo la Amani katika Shehia zilizoko katika Jimbo hilo Mwakilisho wa Masheha wa Jimbo hilo, wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Amani.,  Tawi la CCM Amani  Sheha wa   Balozi Seif akimkabidhi Vifaa vya Miundombinu ya Ujenzi Mmoja Miongoni mwa Masheha waliomo ndani ya Jimbo la Amani kwa ajili ya Shehia zao.
Na.Othman Khamis.OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewathibitishia Wananchi wote kwamba Serikali Kuu itazidisha nguvu zaidi katika kusimamia Amani iliyopo Nchini ili kuongeza kasi ya Maendeleo yaliyoshamiri kila pembe ya Taifa hili.
Alisema nguvu hizo zitakwenda sambamba na kupiga vita chechea zitakazoashiria muelekeo wa uvunjifu wa Amani inayohitaji kutumia gharama kubwa kuirejesha pale inapoterereka ambayo Taifa kamwe lisingependa kutokea.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa thibitisho hilo wakati akitoa salamu kwenye Mkutano wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ulioitishwa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Amani Maalim Mussa Hassan na Mh. Rashid Ali Juma mara baada ya uzinduzi wa Awamu ya Mwanza ya Matengenezo ya Tawi la CCM Kwawazee.
Alisema Zanzibar imepata mabadiliko makubwa Kiuchumi ndani ya Kipindi cha Miaka Mitano yaliyosaidia kustawisha hali za Wananchi wake kutokana na utekelezaji mahiri wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2015 – 2020 uliosimamiwa na SMZ chini ya Rais wake Dr. Ali Mohamed Shein.
Balozi Seif alitanabahisha kwamba ili Wananchi waende sambamba na kasi hiyo ya Serikali Kuu kwa upande wao lazima wafanye kazi kwa bidi ya Kujenga Nchi kwa kuudhihirishia Ulimwengu mafanikio hayo na kuwaacha wale wasiokwisha jibebesha lawama wakiendelea kuweweseka muda wote.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwakumbusha Wananchi wapenda Maendeleo kutenga muda Maalum wa kuyatangaza mafanikio yaliyopatikana katika Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi njia itakayozima upotoshwaji wa makusudi wa mafanikio hayo unaofanywa na baadhi ya Watu kwa utashi wao.
Balozi Seif ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Aman Maalim Mussa Hassan na Mwakilishi wa Jimbo hilo Mh. Rashid Ali Juma kwa usimamisi wao imara wa Ilani ya Uchaguzi ndani ya Jimbo lao.
“ Hili la Ujenzi wa Tawi lenu la Chama cha Mapinduzi la Kwawazee limetia fora likienda sambamba na hadhi ya Chama chenyewe kama Uongozi wa Juu unavyoagiza kila mara”. Alisisitiza Balozi Seif.
Alisema usimamizi huo ulioungwa mkono ya Viongozi wa Jimbo hilo kuanzia Ngazi ya Shina umeliwezesha Jimbo hilo kupata mafanikio makubwa ya Maendeleo, Uchumi na Ustawi wa Jamii na kuweka rikodi ya mafanikio ikilinganishwa na Majimbo mengine ndani ya Wilaya na Mkoa mzima wa Mjini Magharibi.
Wakielezea Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 ndani ya kipindi cha Miaka Minne Mbunge wa Jimbo la Amani Maalim Mussa Hassan na Mwakilishi wa Jimbo hilo Mh. Rashid Ali Juma walisema kazi hiyo tayari imeshafikia asilimia 90% ya Utekelezaji wake.
Walisema asilimia 10% iliyobakia ambayo iligusa zaidi katika Sekta ya Michezo tayari imeshapatiwa ufumbuzi wake kutokana na Jimbo hilo kubarikiwa kuwa na Timu Nane za Soka zikiwa shinashiriki Ligi Dajara la Kwanza Kanda linalohitaji huduma kubwa zaidi ikilinganishwa na Madaraja mengine.
Maalim Mussa Hassan na Mh. Rashid Ali walifafanua kwamba Miaka Minne ya Utekelezaji wa Ilani hiyo ya Uchaguzi ilijikita katika Sekta ya Elimu, Miundombinu ya Bara bara katika Kiwango cha Kifusi, Huduma za Maji Safi na Salama, Uwezeshaji Kiuchumi pamoja na Huduma za afya ambazoWananchi wa Jimbo hilo wanaringia uwepo wa Kituo cha Afya kinachotoa huduma saa 24.
Walieleza kwamba hayo yamepatikana na kufanikiwa kutokana na Ushirikiano wa karibu kati ya Uongozi wa Jimbo pamoja na Wananchi wake hali iliyopelekea ushawishi wa kutumika kwa zaidi ya Shilingi Milioni 325,000,000/- zilizotokana na Mifuko ya Jimbo ya Mbunge na Mwakilishi pamoja na fedha zao Binafsi Viongozi hao.
Mapema akimkaribisha Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Mjini Nd. Talib Ali Talib alisema Uongozi wa Mkoa huo umekuwa shahidi kuona Utekelezaji mkubwa wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ndani ya Jimbo la Amani aliopelekea kuondosha Kero nyingi zilizokuwa zikiwakabili Wananchi wake.
Nd. Talib alisema wapo baadhi ya Watu wachache wanaotaka kufarakanisha Viongozi hao waliokwishaonyesha uwezo mkubwa wa kuwatumikia Wananchi waliokubali kuwapa ridhaa ya kuwaongoza.
Alisema Chama cha Mapinduzi Mkoa Mjini kitaendelea kumuheshimu Mtu yeyote mwenye nia thabiti ya kuona Ustawi wa Wananshi unaimarika zaidi na yule atakayekuwa hayawani wa kubeza Maendeleo yaliyopatinaka ndani ya Mkoa Uongozi huo utakuwa tayari kupambana na Mtu huyo kwa nguvu zote.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauti Kuu ya Taifa ya CCM katika shughuli hiyo alipata fursa ya kukabidhi Vifaa mbali mbali kwa ajili ya Wananchi wa shehia Nne zilizomo ndani ya Jimbo la Amani.
Vifaa hivyo ni pamoja na vile vya Ujenzi wa  Miundombinu ya Huduma za Maji safi na Salama na seti za Jezi kwa Timu zilizomo Jimbo hilo la Amani ndani ya Wilaya ya Mjini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.