Habari za Punde

Vijana Washauriwa Kuazisha Miradi ya Kilimo cha Mbogamboga

Na.Raiye Vuale -Pemba.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya vijana  Mwanaidi  Mohd Ali,amewataka Vijana kisiwani Pemba kubadilika kwa kutokata  tamaa na kuwa wabunifu kwa kuanzisha bidhaaa ambazo hazijafanywa na wengine ili kukuza Miradi yao.

Mwanaidi alitoa rai hiyo   alipokua akizungumza na vijana wakati wa ziara ya  kukagua vikundi vya vijana wanaojishughulisha na Miradi mbalimbali ya  maendeleo   kisiwani Pemba.

Akizungumza na vijana wakikundi cha NURU JAMAA wanaojishughulisha na kilimo cha mbogamboga katika kijiji cha shumba Mjini Wilaya ya Micheweni aliwashauri kuanzisha miradi ya kilimo ikiwani njia mojawapo ya kuongeza uzalishaji.

Alisema kutokana na ardhi ya eneo lao la Mawe linastawi mazao mbali mbali  na kuwa ahidi kuwaletea wataalamu waliopata mafunzo ya fursa kijani waweze kuwasaidia mbinu zitakazosaidia katika uzalishaji na kuboresha mazao wanayozalisha.

“Eneo hili linastawi mazao mbali mbali , hivyo nawashauri muazishe miradi ya kilimo na naahidi kuwaletea wataalamu kwa ajili ya kuwasaidia kufikia malengo yenu”alisema.

Aidha amewashauri Vijana wa kikundi cha TUKOTAYARI katika kijiji cha Michungwani Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba kuanzisha Biashara ya Boda boda ili kuisaidia jamii yao kuepuka kutembea kwa masafa marefu kutoka na kutokuwepo kwa usafiri unaokwenda kijijini kwao.

Aliwasisitiza vijana hao kuweka kipaumbele katika kufatilia mahitaji ya shughuli wanazozifanya ili waweze kuharakisha maendeleo ya vikundi vyao.
Pia  Mkurugenzi huyo aliwataka vijana kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali pamoja na taasisi binafsi kama kupatiwa mikopo, elimu na vifaa vya uzalishaji kwa lengo la kujikwamua na kujiendeleza kimaisha.

Nae Mratib idara ya Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Haji Khamis Haji aliwaeleza vijana njia na Masharti ya kupata Mkopo kulingana na shughuli zao na jinsi ya kurejesha mikopo hiyo, ikiwa ni njia ya kuwawezesha wajasiriamali ambao ndio lengo la mfuko wa uwezeshaji.

Alisema mfuko wa uwezeshaji ni katika jitihada za serikali kuona vijana wanajiajiri unanufaisha wakulima, wasafirishaji, wasarifishaji na wauzaji matunda na mbogamboga. Ambao ni mkopo mdogo.

Mratibu wa Idara ya Maendeleoya Vijana Pemba Ali Mussa Bakar amewahimi za vijana kuwa tayari kujitolea na kufanyakazi kwa maendeleo ya kikundi na wao binafsi.

Afisa ushirika wilaya ya chakechake amewataka vijana kuwa makini katika uwekaji wa kumbukumbu wanapofanya shughuli zao kwa lengo la kukuza maendeleo ya kikundi kwa faida na matumizi ya baadae.

Katika ziara hio ya siku nne iliyofanyika katika wilaya zote za Pemba ambayo ilianza katika wilaya ya Mkoani Mkoa wa kusini Na kumalizia katika wilaya ya ChakeChake Mkoa wa Kusini Pemba nakutembelea Jumla ya vikundi 20 kwa idadi ya vikundi 5 kwa kila wilaya.

Ziara hiyo ilikua na lengo la kujua mafanikio na changamoto mbalimbali zinazowakumba vijana ili kuweza kuwasaidia njia tofauti za kuweza kuzitatua.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.