JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI
TANZANIA

TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
KAMISHNA
WA OPERESHENI NA MAFUNZO CP
SABAS, AMEAGIZA GODBLESS LEMA (MB) ATAFUTWE NA AKAMATWE POPOTE ALIPO KWA TUHUMA
ZA KUTOA TAARIFA ZA UONGO
Ndugu
Wanahabari,
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas, mapema jana
amewasili mkoani Singida na kutoa ufafanuzi wa matukio ya mauaji ya watu 14
yaliotokea mkoani humo wilayani Manyoni kuanzia mwaka jana mpaka kwaka huu
mwezi wa pili.
Aidha katika kutoa ufafanuzi huo Kamishna
CP Sabas alisema taarifa hizo za uongo ambazo zilisambazwa na Mbunge wa
Arusha, Godbless Lema huku akimtaka kujisalimisha katika kituo chochote cha
Polisi, huku akitoa maagizo kwa Kamanda Polisi Mkoa wa Singida kumtafuta Mh
Lema popote alipo na akamatwe.
Kamishna CP
Sabas amesema Mnamo tarehe 29/2/mwaka huu huko katika Wilaya ya Manyoni wakati
wa kutoa salamu kabla ya mazishi ya marehemu Alex Jonas ambaye alikutwa ameuawa
kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake katika
Eneo la Mbugani, Godbless Leama ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini
alionyesha orodha ya watu 14 ambayo pia aliiweka katika mitandao ya Kijamii akidai
waliuawa kwa kuchinjwa Wilayani Manyoni bila ya kuwa na uhakika kama taarifa
hizo ni sahihi huku akilituhumu Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida kushindwa
kutekeleza wajibu wake.
Cp sabas
ameeleza ukweli wa matukio hayo ni kama ifuiatavyo;
1.
Sichelela
Mosses, (22), Mkazi wa Sayuni, tukio
lililotokea tarehe 13/8/2019 majira ya usiku huko maeneo ya Mnarani barabara ya
kuelekea Itigi ambapo Binti huyo alikutwa ameuawa. Baada ya uchunguzi
ilibainika kuwa mauaji hayo yametekelezwa na mume wake aitwaye Rashidi s/o
Hamisi akishirikiana na Timoth s/o Leonard, sababu ikiwa ni wivu wa mapenzi kwa
kumtuhumu mkewe kuwa na mahusiano ya kimapenzi watu wengine. Watuhumiwa wote
wawili wamekamatwa pamoja na vielelezo vyote vilitumika kwenye mauja hayo.
2.
Abdallah
Lyama, (38), Mkazi wa Kihanju, Itigi,
alifariki dunia tarehe 26/8/2019 saa 2 usiku wakati akiendelea na matibabu
katika Hospitali ya St. Gaspar Itigi, Wilayani Manyoni kutokana na shambulio la
kupigwa kwa fimbo pamoja na mateke na ngumi sehemu mbalimbali za mwili wake na
Rajabu s/o Juma, Msambaa, (42) akishirikiana na Haruna s/o Hamisi, kwa pamoja
walikuwa wanamtuhumu marehemu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtoto wa dada
yake Rajabu s/o Juma, aitwaye Asha d/o Miraji, Msambaa, (19). Tukio hilo
lilitokea tarehe 25/8/2019 huko maeneo ya Mji Mpya, Itigi walipomvizia marehemu
akiongea na Binti huyo kichochoroni. Mtuhumiwa Rajabu s/o Juma amekamatwa na
juhudi za kumtafuta mwenzake zinaendelea.
3.
Rajabu
Abasi, (36), alifariki dunia tarehe 14/9/2019
usiku akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya St. Gaspar, Itigi kutokana
na tukio la kuchomwa na kitu chenye ncha kali na mtuhumiwa aitwaye Mohammed Abdi, tukio lililotokea tarehe
13/9/2019 saa 3 usiku huko katika Kijiji cha Mwamagembe. Chanzo cha tukio hilo
ni wivu wa kimapenzi ambapo mtuhumiwa alimfumania marehemu akiwa na mke wake
nyumbani kwa mtuhumiwa. Mtuhumiwa amekamtwa na upelelezi umekamilika.
4.
Martini
Motekwa, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka
30, ambaye inasadikiwa kuwa ana upungufu wa akili na akiwa hana makazi maalum,
mwili wake ulikutwa kwenye kibanda alichokuwa akijihifadhi nyakati za usiku
ukiwa umechomwa moto. Katika uchunguzi mwili huo pia ulibainika kuwa na jeraha
kichwani ambalo linasadikiwa kusababishwa na kitu chenye ncha kali. Bado
uchunguzi wa kuwatafuta watuhumiwa unaendelea
5.
Hamad
Hussein, (37), mkazi wa Manyoni alifariki dunia
baada ya kushambuliwa na wananchi wanaosadikiwa kujichukulia sheria mikononi
kwa kutumia fimbo na mawe kutokana na tuhuma za wizi wa mifugo. Mtuhumiwa mmoja
aitwaye Hussein s/o Mrisho amefikishwa
mahakamani kuhusiana na tukio hilo.
6.
Emmanuel
Meso, (50), Mkazi wa Kijiji cha Maweni,
Tarafa ya Kintinku, alifariki dunia kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu
za siri. Mwili wake uligundulika tarehe 8/11/2019 alifajiri ukiwa umetupwa
porini. Katika uchunguzi wa Polisi imebainika kuwa watu nane wanasadikiwa
kuhusika katika kutenda kosa hilo linalohusishwa na imani za kishirikiana.
Aidha katika tukio hilo yupo Mganga wa Jadi anayesadikiwa kuwatuma watuhumiwa
kuchukua shemu hizo za siri. Watuhumiwa wote wamekamatwa na upelelezi umekamilika,
waliokamatwa ni Abdul Muhengwa, Henry
Madinda, Stephano Ligoha, Juma Kassim, Makayola Gaudence, Regina d/o Jacob,
Wami s/o Ngalya, na Anderson s/o Sabini.
7.
Mika
Saimon, (38), alifariki dunia kwa kukatwa na
vitu vyenye ncha kali katika sehemu mbalimbali za mwili katika tukio
lililotokea tarehe 15/11/2019 saa 10 jioni huko Kitongoji cha Idodoma, Tarafa
ya Nkonko, ambapo marehemu aliuawa na mtoto wake aitwaye Saimon s/o Mika kwa
akishirikiana na mama yake mzazi aitwaye Mea d/o Mwarabu pamoja na rafiki wa mtoto
wake aitwaye Robert Elia ambapo walikuwa wanataka kurithi shamba la baba yao.
Watuhumiwa wote watatu wamekamatwa na upelelezi wa Polisi umekamilika.
8.
Mshoma
Ngassa, (30), Mkazi wa Itigi alifariki dunia
kwa kupigwa kwa fimbo kichwani na mume wake aitwaye Mariyambelele Senzo katika tukio lililotokea tarehe 21/11/2019 saa
2:30 asubuhi huko Majiweni, Kata ya Mitundu ambapo chanzo cha kifo ni wivu wa
kimapenzi ambapo mtuhumiwa akimtuhumu mke wake kutembea na mwanaume ambaye bado
hajafahamika. Mtuhumiwa amekamatwa na upelelezi wa Polisi umekamilika.
9.
John
Logion, (60),
Mkazi wa Mitundu alifariki dunia katika tukio lililotokea tarehe 22/11/2019 saa
11 jioni kwenye shamba la mihogo, lilnalomilikiwa na Anthony Lipiti huko Itigi. Uchunguzi wa awali wa Polisi umebaini
kuwa chanzo cha tukio hilo ni wizi ambapo marehemu alikwenda kwenye shamba la
mtuhumiwa kwa nia ya kuiba mihogo na mtuhumiwa kutumia mwanya huo kumshambulia
kwa kumpiga na kitu kizito kichwani. Mara baada ya tukio mtuhumiwa alitoroka na
juhudi za kumtafuta zinaendelea kwa kushirikiana na Viongozi wa Eeneo husika.
10. Michael Charles,
(35), Mkazi wa Mwamagembe alifariki 1/1/2020 wakati anapatiwa matibabu katika
Zahanati ya Mwamagembe, Itigi kutokana na taarifa za kujeruhiwa na Fatuma d/o
Ramadhani tukio lililotokea tarehe 21/12/2019. Katika tukio hilo inasadikiwa
kuwa Fatumaa d/o Ramadhani ambaye ni Mmiliki wa nyumba aliyokuwa anaishi
marehemu alimpiga kwa jiwe kichwani na kisha kumvuta sehemu za siri kutokana na
ugomvi wa uchafuzi wa mazingira katika eneo la nyumba wanayoishi. Hata hivyo
tukio la kujeruhiwa halikuripotiwa Polisi hadi muathirika alipofariki. Baada ya
tukio la kujeruhi mtuhumiwa alotoroka juhudi za kumtafuta zinaendelea.
11.
Issa Abdallah (2), ambaye alikuwa mlemavu wa miguu alifariki dunia tarehe 24/1/2020
saa 12 jioni huko katika Kitongoji cha Ibonoa, Kata ya Sanjaranda – Itigi
kutokana na kunyongwa na mama yake mzazi kwa kile kinachodaiwa kukosa mahitaji
kutoka kwa baba wa mtoto aitwaye Abdallah s/o Muna, (56), Mnyaturu
aliyemtelekeza bila matunzo. Mtuhumiwa amekamatwa na upelelezi wa Polisi
umekamilika
12.
Jumanne Ndelemo, (22), alifariki
dunia baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali na kaka yake wake aitwaye Hamisi s/o Ndelemo, kutokana na kumfumania
akiwa na mke wake. Tukio lilitokea tarehe 5/2/2020 saa 3:30 usiku huko katika
Kijiji cha Makasuku, huko Sasajila na mtuhumiwa amwekamatwa na upelelezi wa
Polisi umekamilika.
13. Heri Mamba
alifariki dunia baada ya kugongwa na pikipiki yenye namba za usasjili MC 273
CDK aina ya FEKON. Kutokana na uchunguzi wa awali wa Polisi imebainika kuwa
marehemu alikuwa amelewa huku akikatiza barabarani bila kuchukua tahadhari.
Mtuhumiwa Ombeni s/o Chanzi, Mgogo, (35), mkazi wa Chinyika amekasmatwa na
amekiri kutenda kosa hilo na si kuchinjwa kama ilivyodaiwa kwenye malalamiko.
14.
Alex Jonas, (40), dereva bodaboda,
aligundulika kufariki dunia tarehe 26/2/2020 saa 1 asubuhi na Uchunguzi
unaendelea ili kuweza kubaini chanzo cha kifo cha marehemu pamoja na wahusika
wa tukio hilo.
Katika Taarifa
ni za upotoshaji zenye lengo la kuleta taharuki kwa Jamii pamoja na
kuwachonganisha Wananchi na Jeshi lao la Oilisi.
Mwisho Kamishna Sabas amesema kuwa hakuna Mwanasiasa au mtu yoyote
atakaetumia Jeshi la Polisi kama kimvuli cha kujipatia umarufu, huku akiwaonya
anasiasa wanaojifanya kuwa ni wasemaji wa Jeshi la Polisi amewaonya na kusema
kuwa jeshi halitamvumilia mtu au kiongozi yoyote atakaeichafua serikali kwa
namna moja au nyingine.
No comments:
Post a Comment