Habari za Punde

MIAKA 48 imepita, huu ni umri wa mtu mzima naweza kusema kwa sasa, ni sawa na maisha ambayo wananchi wa kijiji cha Mpale ambao wameishi, huku wakiwa ndoto siku moja watapata huduma ya umeme kijijini pao.


MSIMAMIZI wa Mradi wa Umeme wa Jua wa Kmapuni ya Ensol katika kijiji cha Mpale,Erica Jackson akiwaongoza waandishi wa habari wa masuala ya nishati Jadidifu Tanzania kuelekea kwenye mradi huo
 BAADHI ya betri za mtambo wa umeme wa jua zikiwa zimeunganishwa kwa ajili ya kuhifadhi umeme huo,pale hali ya hewa inapokuwa mbaya.
BAADHI ya mitambo ambayo hutumika katika kusambazia umeme wa jua na kuhifadhia ili kupeleka kwa wananchi kiwango sahihi, ikiwa ndani ya mtambo wa umeme wa jua wa kampuni ya Ensol katika kijiji cha Mpale.
VIOO vya umeme wa jua vikiwa vimetandazwa katika nguzo maalumu, kutoka kampuni ya Ensol huko katika kijiji cha Mpale Wilaya ya Korogwe.
(PICHA NA ABDI SULEIMAN)

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.
Kijiji cha mpale kilianzishwa mwaka 1972, tokea mwaka huo suala la huduma ya nishati ya umeme ilikuwa ni ndoto, kitendawili kilichokaa kwenye vichwa vya wanakijiji.
Mpale ni miongoni mwa vijiji vinne vilivyomo katika kata ya mpale, vijiji wenyewe ni Mali, Tewe, Kwamanolo na Mpale, ambapo kila kata hiyo inavitongoji 20 huku kila kijiji kina vitongoji vitano.
Kata ya mpale imo katika tarafa ya bongo wilayani Korogwe katika Mkoa wa Tanga, ambapo lazima kijasho kikutoke na ujipange wakati ukijianda kwenda katika kijiji cha Mpale.
Kijiji cha mpale ni moja wapo wa vijiji vinapatikana katika milima iliyopo wilayani Korogwe, huku kikiwa na mazingira mazuri ya hali ya hewa muda wote ikiandamwa na ubaridi baridi.
Mwandishi wa makala haya kwa udhamini Chama cha waandishi wa habari za mazingira Tanzania (JET), wakishirikiana na kampuni ya habari na Teknolojia ya NUKTA Afrika na shirika la HIVOS, aliweza kufika katika kijiji cha Mpale na kuangalia mafanikio na changamoto za nishati ya umeme wa jua, ambao ni miaka mitatu tu tokea kuwekwa kijijini hapo.
Kata ya mpale ina jumla ya wananchi 9613, wanawake 4312 wanaume 5301, wazee 684 wanaume 261 na wanawake 423, shuhuli kuu za wananchi ni kilimo na ufugaji.
Kwa mujibu wa Malengo Endelevu ya Dunia SDGs, lengo namba (7)linalohusiana na masuala ya nishati, limesema katika mwaka 2000 nadi 2016 ididi ya watu walio na umeme, iliongezeka kutoka asilimia 78 hadi 87, kadri ya watu wanavozidi kuongezeka ndivo nishati ya bei rahisi inavyohitajika.
Wakati umefika kuwekeza katika nishati ya jua, umeme wa upepo na mafuta, ili kuboresha hali ya uzalishaji wa nishati na kuhakikisha nishati muda wote inadumua.
WANANCHI WANASEMAJE JUU YA NISHATI
Mahunge Mussa Mkande ni mfanyabiashara wa Duka, umeme huu umeweza kubadilisha maisha ya wananchi wa kijijini, kwenye shuhuli za kiuchumi, tafauti na mwanzo maduka tulikuwa tunafunga saa 12 za jioni, sasa tunafika saa nne usiku bado maduka yako wazi.
Amesema matumizi ya umeme kijijini umeweza kuongeza kipato kwa wafanyabiashara, tafauti na walipokuwa wakifanya biashara kwa kutumia taa za vibatari.
“Huu umeme wa jua ni wa uhakika na mzuri, haukatiki mara kwa mara kama umeme wa REA, umeweza hata kupandisha bishara baada ya kuweka friji dukani kwake”alisema.
“kuwepo kwa friji dukani kwake, kumepelekea mapato kuongezeka kwa siku anauza kati ya elfu 70,000/=hadi 80,000/=, jambo ambalo tafauti na kabalaya kuwepo kwa umeme akiuza shilingi elfu 50,000/= kwa siku”aliongeza.
Aidha Mahunge amesema umeme huo umemfanya kuweka banda la kuonyesha TV kwa wananchi, ambapo kiingilio ni shilingi 300 hadi 500 kwa baadhi ya michezo, huku mpira kwa mtu ni shilingi 1000 kwa mechi moja.
Mohamed Hashim mlale mmiliki wa mtambo wa kujazia upepo katika kijiji cha Mpale, alisema kuwepo kwa umeme huo umeweza kutoa ajira kwa vijana kijijini, vijana wengi wameweza kuingia katika biashara mbali mbali ikiwemo bodaboda.
Baada ya kuja kwa umeme huu, alilazimika kuweka mtambo wa kujazia upepo, ili kuwaondoshea usumbufu waendasha bodaboda kijijini, kufuata huduma hiyo masafa ya mbali na wengine kufika mjini, ambapo kwa siku hukusanya kati ya elfu 15,000 hadi 20,000/=.
“Kuwepo kwa mtambo huu nimeweza kuajiri hata vijana wawili kijijini, kwa shuhuli za kujaza upepo pikipiki na baadhi ya magari, pia napata cha kuwalipa vijana hawa kwa siku”alisema.
Philips John Yohana kijana aliekeza katika utoaji wa huduma za saluni, amesema baada ya kuja kwa umeme Ensol alilazimika kuanzisha saluni, kwa ajili ya kujikwamua na hali ngumu za maisha.
Amesema kazi yake imeweza kumpatia kipato cha kujikimu kimaisha, kwa siku hukusanya kati ya elfu 15000 hadi 20,000/=, jambo ambalo limemuepusha na ukaaji wa vijiweni.
WAACHANANA MATUMIZI YA NISHATI MAFUTA.
Mwanahija Rajab Shomar alisema uwepo wa umeme wa jua kijiji kwao, ameweza kuachana na matumizi ya nishati ya mafuta ya taa, wakati mafuta akitumia robo kwa siku tatu.
“Mimi nilikuwa nalipa shilingi 800 napata robo ya mafuta, kuja huu umeme na mimi nimekubali kuungiwa na wanangu hawasomi tena usiku kwa koroboi”alisema.
Umeme unachangamoto kubwa tunalipa kwa kifurushi, kwa mwezi 11000 hata 5000 au 2000 unaweza kupata kifurushi chako.
Rashid Haidar alishukuru kuweka umeme kijijini, wananchi wengi wengi wameweza kuunganisha kitu ambacho walikuwa wakikisubiri kwamuda mrefu.
Amsesema alikuwa kilazimika kununua mafuta ya taa ya shilingi 2800 lita moja, ili kutumia kwa wiki nzima wakati mwengine mafuta yanaisha hata wiki haijafika.
Yakub Shomari ambaye ni mfanyabiashara, kwa mwezi akitumia lita tano za mafuta hayo, lita moja ni 2700 sawa na shilingi 13500, huku mwaka mmoja akitumia shilingi 162000 kwa kununulia mafuta ya taa.
“umeme wa jua kijijini kwetu umeanza kutoka huduma kwa wananchi 2017, sasa ni miaka mitatu ningekuwa nimeshapoteza shilingi 48600, umeme huu ninaolipa 11000 kwa mwezi na mwaka ni shilingi 132000, kwa miaka mitatu tokea kuanza nimelipa shilingi 396000, nikiwa nimeokoa shilingi 90000 kwa mwaka”amesema.
Hata hivyo amesema miaka 48 wametumia nishati ya mafuta, hata wanafunzi walikuwa wanapata tabu kusoma masomo ya ziada muda wa usiku, umeme huo umeweza kurahisisha hata maendeleo kwa mtu mmoja mmoja.
           MWALIMU WA SKULI NA WANAFUNZI WANASEMAJE
Mwalimu Mkuu skuli ya msingi Mpale, Humphrey Mhina amesema umeme ulianza 2017, mwanzo walikuwa na shida sana walikuwa wakiogopa hata kufikaa skuli usiku kusaidia wanafunzi, hata simu wakichaji majumbani kwaa kutumia sola.
“Wakati mwengine tulishindwa hata kufundisha wanafunzi, kutokanana skuli ilijengwa kwa kutumia miundombinu ya kizamani, madirisha hayapitishi mwanga ndani, wakati mwengine ukungu ukitanda inakuwatabu kusomesha, sasa umeme upo tunawasha taa mambo yanasonga mbele”amesema.
Amesema kuwepo kwa umeme wamelazimika kuanzisha madarasa ya usiku kwa wanafunzi, ili kuwasaidia wanafunzi hata ufaulu umeongezeka kwa waliofanya mitihani darasa la nne kuingia la tano, walikuwa wanafunzi 263 kutokana na jitihada za umeme usiku 234 wamefaulu kwenda la tano.
“Mwanzo wanafunzi walikuwa hawajuwi kusoma na kuandika sasa wanaweza kusoma, kama kusingekuwaa na umeme wangefelisha wanafunzi wengi, umeme umewafanya hata walimu kupenda mazingira haya, tokea mwaka 2017 hakuna walimu waliohama tena kijijini hapa”amesema.
Mwanafunzi Daudi Ahmed STD 7, amesema huduma ya umeme umeweza kuwahamasisha kupenda kusoma hata muda wa usiku masomo ya ziara, ambayo yalikuwa hayapo skulini pao.
Hidaya Abass anaesoma darasa la tano, umeme umepelekea kuama hata muda wa usiku kujisomea, zaidi pale anapokabiliwa na mitihani hukaa kambini na wenzake.
KWAU UPANDE WA AFYA UMEME UKOJE
Mganga mfawidhi Zahanati ya Mpale, Herman Magembe amesema umeme umewasaidia kwa kiasi kikubwa, kuboresha huduma za afya ikiwemo suala zima la chanjo, pamoja na huduma za mama na mtoto, akinamama wameondokana na tatizo la kujifungulia usiku kwa kutumia tochi na koroboi.
“Mwanzo kabla ya umeme tulikuwa tunatumia friji la gesi, tena ikajazwe korogwe, vifaa kuchemsha mpaka tuweke kuni au mafuta, wakati mwengine usiku unatumia tochi yako ya nyumbani kuzalishia, mungu ametusaidia hakuna vifo tu”alisema.
Herman amefahamisha umeme umeweza kuwasaidia sana, kwa mwezi wanalipa elfu 36000, wakati kabla wakitumia elfu 60000 kwa mwezi, sasa watu 30 hadi 35 wanajitokeza kwa mwezi kujifungua.
VIONGOZI WA MRADI YEYE ANASEMAJE
Afisa msimamizi wa mradi wa umeme wa jua kijijini Mpale, Erica Jackson amesema kijiji kilianzishwa mwaka 1972, tokea mwaka huo huduma ya umeme imepatikana mwaka 2017 baada ya kampuni ya Ensol kujitolea kupeleka na kuanza na wateja 61 na hadi sasakuwana wateja 250.
“Kupitia REA tumeweza kupunguzia gharama za wearing kwa asilimia 40, pawer Africa aliwadhamanini wananchi kuwapatia wearing na kurudisha ndani ya miaka miwili, kila mteja ametolewa laki mbili kwa kukopeshwa na analipa kidogo kidogo na lengo limefikiwa”amesema.
Umeme huo umeweza kuzalisha zaidi ya biashara 20 mbali mbali kijijini hapo, zikiwemo nyumba za ibada, skuli, hospitali, changamoto kubwa ni miundombinu sio mizuri kufika kijijini, hususana kipindi cha mvua, pamoja na marejesho ya wearing kutokurudishwa kwa wakati, ikizingatiwa kipato cha wananchi ni chamsimu.
“Huu ni umeme wa kifurushi na bei ni 11000, 20000, 36000, 53000, 70000, mapaka laki 104000/= lakini wananchi wengine wa majumbani wanatumia kifurushi cha 11000/=.
“Sasa tunazalisha 48KWT kwa matumizi ya majumbani, matarajio yetu ni kuzalisha uniti 240 kwa siku, iwapotukiwa na viwanda kama vya chai, miwa, umeme huu unategemea na matumizi yako ndio unavozalisha”
Amefahamisha kuwa kasi ya watu kujiunga ipo kwa 40% kwa mwaka 2019, ukiunganisha na umeme wa REA unavokatika hususan kipindi cha mvua na upepo, ambapo jumla ya Bilioni 1 imetumika kugharamia mradi huo.
VIONGOZI WA SERIKALI WANAYAPI WAO
Mtendaji wa kata ya Mpale Mwanahija Abdalla Nurdin, alishukuru kupata umeme wa Ensol kijijini kwao na kuanza kubadilisha maisha ya wananchi, kwani umeme hurahisisha maendeleo ya sehemu yoyote ile.
Amesema umeme huo umesababisha watu kuanzisha biashara mbali mbali, wananchi wa kujiajiri huduma za afya kutolewa mpaka muda usiku, ikiwemo wazazi kujifungulia bila ya tabu na hofu kwa sasa.
“Uchumi umeendelea kukukuwa kwa wanafanyabiashara sasa wanafika mpaka saa nne usiku, baada ya saa 12 za jioni kabla ya umeme, pamoja na woga wa wananchi pia umewaondoka”alisema.
Mwenyekiti wa serikali yakijiji cha Mpale bdalla Mohamed Mdowe, Umeme umewatoa katika giza kwa kusubiri umemewa REA, watoto walikuwa wakisoma kwa kutumia vibatari sasa umeme, skuli wanasoma mpaka usiku, huku zahanati wakitumia karabai wakati wa kujifungulia sasa wanatumia umeme wa kawaida.
HITIMISHO
Licha ya wananchi wa kijiji cha Mpale kufikiwa na umeme wa ensol, lakini bado wananchi wengi wameshindwa kuunga umeme huo kutokana na kuwa nagharama kubwa, ukilinganisha na umeme wa REA unaonunua kwa uniti, ipo haja kwa serikali na mashirika maengine kuelekeza nguvu zao katika kusaidia huduma ya nishati katika kijiji cha mpale, kilichopo tarafa ya Bongo Wilayani Korogwe Mkoani Tanga.
MWANDISHI WA MAKALA HAYA SIMU 0718 968355.
EMAIL:abdisuleiman33@gmail.com
MWISHO

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.