Habari za Punde

Uzinduzi wa Kikundi cha Wajasiriamali cha Wapendanao Zanzibar.

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe.Mahmoud Thabit Kombo akikata Utepe kuashiria Uzinduzi wa Kikundi cha Wajasiria mali cha Wapendanao Kwa mchina mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Wajasiria mali (WAPENDANAO)akisisitiza jambo alipotoa hatiba yake katuika hafla ya Uzinduzi wa Kikundi hicho Kwamchina mjini Zanzibar.
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Kikundi cha Wajasiria mali cha Wapendanao Kwa mchina mjini Zanzibar.
Picha na Fauzia Mussa - Maelezo  Zanzibar.

Na Mwashungi Tahir   10-3-2020.
WAZIRI wa Habari Utalii na Mambo ya Kale ambaye pia ni mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo amevitaka vikundi vya wajasiriamali kuwa na mashirikiano  katika utendaji wa kazi zao ili kuleta ufanisi zaidi.
Ameyasema hayo huko katika Tawi la Kiembe samaki  kwa Mchina wakati alipokuwa akizindua kikundi cha wajasiriamali cha wapendanao na kuwataka wajenge tabia ya kushirikiana ili waweze kufanya kazi kwa mafanikio zaidi.
Amesema kikundi cha wapendanao ambacho kinakwenda sambamba na siku ya wanawake duniani kikiwa na lengo cha kuhamasishana katika utendaji wao kwa kuweza kusaidiana  na kupata maendeleo.
Aidha amesema iwapo kikundi hicho kitakuwa na mashirikiano kinaweza kudumu kwa muda mrefu  na kuwataka kuiga mfano wa  kikundi cha saccos  meli nne ambacho kiko imara kimekuwa  kinasonga mbele na  kupata  maendeleo makubwa.
“Nawaomba mujenge mashirikiano yaliyo mazuri ili kikundi hichi kiweze kudumu na mfano muige katika kikundi cha saccos meli nne jinsi kilivyodumu kwa muda mrefu na kina akiba ya kutosha hadi kufikia kukopeshana”, alisema mwakilishi huyo.
Hata hivyo amesema alitaka muhasibu kuwa makini katika utoaji na uingizaji wa fedha ili kuondosha migogoro kutokea na kuweza kuvunja nguvu za maendeleo waliyojipangia kikundi hicho.
Vile vile Mwakilishi wa jimbo hilo ambae pia ni Waziri wa Habari Utalii na mambo yaKale aliwasa tabia ya wanavikundi kukaa kusemana nje ya vikundi visivyo rasmin kwani kufanya hivyo kunachangia kutetereka kwa vikundi hivyo.
Kwa upande wa wanakikundi hao cha wajasiriamali  cha wapenda nao wamekabidhi risala kwa kutaka wasaidiwe fedha kiasi cha shilingi milioni kumi ambazo zitaweza kuimarisha kikundi hicho kwa kufanya mambo mengi ya utendaji wa kikundi chao.
Pia wamesema kikundi hicho kimeanzishwa na wanachama 14 wanawake watupu  katika  mwaka 2016 kwa lengo la kufuatia wito wa Serikali na Chama cha Mapinduzi kwa kuhamasishana umoja , mshikamano na mashirikiano baina ya   wanachama .
Wamesema Malengo yao makuu ni kuongeza nguvu , kuona wanawake wanapambana na kupinga  vitendo vya udhaliishaji kwa wanawake na watoto   ambavyo vimekithiri hivi sasa na waweze kujitegemea na kuacha kuwa tegemezi kwa kina baba .
Wakitoa changamoto zinazowakabili wamesema wana ukosefu wa jengo la kudumu pia wana uhaba wa elimu ya kutosha katika masuala ya ubunifu wa ujasiriamali .
Kwa upande wa mafanikio wameweza kuchangishana fedha kila mwisho wa mwezi kwa lengo la kutunisha mfuko wao na kuweza kukopeshana baadhi ya huduma mbali mbali ikiwemo vitenge na mambo mengine na kusaidiana  pale wanapopata tatizo.  
Nae Katibu wa kikundi  cha wapendanao Fatma Ibrahim Khamis amesema kikundi hicho kina matarajio ya kuwanyanyua na kuwaweka wanawake  kuwa kitu kimoja  katika kujiletea maendeleo katika harakati za jamii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.