Habari za Punde

Wananchi wa Kata ya Mpale Kuachana na Nishati ya Matumizi ya Mafuta ya Taa na Kutumia Nishati ya Umeme wa Jua

NA ABDI SULEIMAN.
WANANCHI 250 kati ya 9613 wa kata ya Mpale, wameamua kuachana rasmi na matumizi ya nishati ya Mafuta ya Taa, badala yake wanatumia nishati ya umeme wa jua wa grid uliopo katika kijiji cha Mpale.
Kata mpale ina vijiji vine, ikiwemo Mpale, mali, Tewe na Kwamanolo, huku ikiwa na jumla ya Vitongoji 20 na kila kijiji kina vitongoji vitano.
Wakizungumza na Mwandishi wahabari hizi baadhi ya wananchi wa kata hiyo, wamesema wamelazimika kuachana na matumizi ya nishata ya mafuta ya Taa, ambayo walikuwa wakiyatumia kwa muda mrefu baada ya kukosekana kwa nishati ya umeme wa uhakika.
Baadhi yao walisema walikuwa wakitumia lita tano kwa mwezi, wakatilita moja ni shilingi 2700, huku wengine wakitumia lita moja kwa wiki, kulingana na matumizi ya mtu nyumbani kwakwe.
Mahunge Mussa Mkande ambaye ni mfanyabiashara, alisema kwa mwezi alikuwa alikuwa akitumia lita tano za mafuta hayo, ambapo lita moja ni 2700 sawa na shilingi 13500, huku mwaka mmoja alikuwa akitumia shilingi 162000 kwa kununulia mafuta ya taa.
“umeme wa jua kijijini kwetu umeanza kutoka huduma kwa wananchi 2017, sasani miaka mitatu ningekuwaa nimeshapoteza shilingi 48600, lakini umeme huu ninaolipa 11000 kwa mwezi na mwaka ni shilingi 132000, kwa miaka mitatu tokea kuanza nimelipa shilingi 396000, nikiwa nimeokoa shilingi 90000 kwa mwaka”alisema.
Alisema matumizi ya mafuta yalikuwa akitumia kwakutokuwa na lakufanya tu, lakini matumizi ya umeme ndio jambo la msingi nabora zaidi kwa sasa.
Hata hivyo alisema miaka 48 wametumia nishati ya mafuta, hata wanafunzi walikuwa wanapata tabu kusoma masomo ya ziada muda wa usiku, lakini umeme huo umeweza kurahisisha hata maendeleo kwa mtu mmoja mmoja.
Mwanahija Rajab Shomar alisema uwepo wa umeme wa jua kijiji kwo ameweza kuachana na matumizi ya mafuta ya taa, japo kuwa mafuta alikuwa akitumia robo kwa siku  tatu.
“Mimi nilikuwa nalipa shilingi 800 napata robo ya mafuta natumia kwa siku tatu, lakini kuja huu umeme na mimi nimekubali kuungiwa na wanangu hawasomi tena usiku kwa koroboi”alisema.
Aidha alisema changamoto kubwa ni ulipaji wa huu umeme kwa kifurushi, kwa mwezi 11000 lakini hata 5000 unaweza kupata kifurushi  chako.
Rashid Haidar alishukuru kuweka umeme kijijini kwao, kwani wananchi wengi wengi wameweza kuunganishiwa kitu ambacho walikuwa wakikisubiri kwamuda mrefu.
Alisema alikuwa kilazimika kununua mafuta ya taa ya shilingi 2800, lita moja ili kutumia kwa wiki nzima wakati mwengine mafuta yanaisha hata wiki haijafika.
Afisa mtendaji wa kata ya Mpale Mwanahija Abdalla Nurdin, alisema kata ya mpale wananchi 9613, wanawake 4312 wanaume 5301, wazee 684 wanaume 261 na wanawake 423, huku umeme wa Ensol umeweza kuwasaidia kuondokana na matumizi makubwa ya taa za koroboi.
Alisema kwa sasa licha ya baadhi ya vijiji kuwanishati hiyo haijafika, lakini wananchi wengi wameachana na matumizi ya mafuta ya taa tokea kuwepo kwa umeme wa nishati ya jua.
Afisa msimamiziwamradi Erica Jackson, alisema kijiji cha mpale kilianzishwa mwaka 1972 tokea kuanzishwa kijiji hichi hakikuwahi kupata huduma ya umeme, hadi mwaka 2017 kampuni ya Ensol ilipo wekeza huduma hiyo baada ya kupewa ruhusa na REA.
Alisema tayari project hiyo ya umeme wa jua imeshabeba tunzo mwaka 2018, huku wannanchi wakitumia umeme huo kwa matumizi ya majumbani, biashara ndogondogo, huku wakiwa na matarajio ya kuzalisha KWT 240 kwa siku iwapo matumizi yataongezeka.
Aidha alisema kasi ya wananchi ya kujiunga na umeme huo ipokubwa kwa 40%, ikilinganishwa na umeme wa REA kitucha pekee umeme wa sola haukati hata kuwe na hali ya hewa mbaya, umeme huo utakuwepo na wananchi wanaendelea kupata hudumahiyooo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.