Habari za Punde

BARAZA LA VIJANA LA ZANZIBAR LAKABIDHI VIFAA KWA SHEHIA MBALI MBALI ZA MJINI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA CORONA

Mwenyekiti wa baraza la vijana Zanzibar akikabidhi vifaa kwa wenye viti wa baraza la vijana wa shehia mbali mbali ikiwa nimsaada wa mapambano dhidi ya virusi vya Corona, hafla iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mjini kwa wazee Zanzibar.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana  Zanzibar Khamis Rashid Kheri akiwasisistiza Vijana  wafuate maelekezo yanayotolewa na Serikali na wataalamu wa Afya juu ya mapambano dhidi ya Corona,katika hafla ya makabidhiano ya vifaa vya mapambano dhidi ya virusi ya Corona huko ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kamati ya mradi wa usafi wilaya Mjini Salmini Mussa akizungumza na wenye viti wa Baraza la vijana  wa shehia za Wilaya ya Mjini kuhusiana na mapambano dhidi ya homa ya mapafu wakati wa makabidhiano ya vifaa vya  kukabiliana na maradhi hayo, (kuliani kwake ) ni Mwenyekiti wa baraza la vijana Zanzibar Khamis Rashid hafla iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mjini Kwa wazee Mjini Zanzibar.
PICHA NA FAUZIA MUSSA /MAELEZO

Na Kijakazi Abdalla   Maelezo   29/04/2020
Jamii imetakiwa kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha janga la maradhi ya covid 19 linamalizika nchini.
Hayo ameyasema Mwenyekiti Baraza la Vijana Zanzibar Khamis Rashid Kheir (Makoti) huko Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mjini Amani wakati akikabidhi vifaa vya kujikinga na maradhi ya corona ikiwemo ndoo na sabuni kwa Shehia 15 za Wilaya ya Mjini Unguja.
Amesema janga la maradhi ya corona linahitaji nguvu za pamoja na kuzidisha juhudi za kujikinga na ugonjwa huo ili kuweza kutokomeza na sio kuliachia Serikali pekee yake kwani limekuwa likiathiri uchumi wa taifa.
Mwenyekiti huyo amewataka Wenyeviti wa mabaraza la vijana katika shehia kutoa elimu kuhusiana na janga hilo jamii jinsi ya kupambana na ugonjwa huo ili usiendelee kuenea kwa kasi nchini
Aidha Mwenyekiti huyo amewasisitiza wananchi wenye uwezo kuendelea kuchangia katika mfuko wa covid 19 ili kuweza kuokoa maisha ya wananchi walioathirika na maradhi hayo.
Hata hivyo ameiomba jamii katika kipindi hichi cha mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani kuomba dua ili kuhakikisha maradhi hayo yanaondoka.
Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Mradi wa Usafi Baraza la Vijana Wilaya ya Mjini Salmin Mussa Nahoda amewaomba wenyeviti wa Mabaraza hayo kuhakikisha kuwa vijana wanafuata maelekezo yanayotewa na Wizara ya Afya.
Hata hivyo amesema kumekuwepo na baadhi ya vijana katika Shehia kutofuata maelekezo yanayotolewa na Wizara ya Afya kwa kujikusanya pamoja katika michezo mbalimbali.
Wakipokea vifaa hivyo Wenyeviti wa Mabaraza ya Vijana Katika Shehia wameiomba Serikali kutoa elimu ya maradhi ya corona kwa kuwatumilia Mabwana afya kupita kila Shehia.
Aidha wamewataka vijana kuondoa dhana ya kuwa ugonjwa huo unawakumba zaidi watu wazima na watoto wadogo, kwani ugonjwa huo hauchagui unawapata watu wa rika zote.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.