Habari za Punde

Nchi zinazoongozwa na wanawake wametumia mikakati gani kukabiliana na janga hili?

 Chansela Merkel anachukuliwa na wengi kama "Shujaa wa Ulaya" katika mapambano dhidi ya virusi vya corona
Wanawake viongozi ambao wamechukua hatua za haraka kukabiliana na ugonjwa wa corona
Kuanzia New Zealand hadi Ujerumani,Taiwan au Norway, baadhi ya nchi zinazoongozwa na wanawake zimeonyesha kuwa na idadi ndogo ya vifo kwasababu ya ugojwa wa Covid-19.
Na wanasiasa wa nchi hizo wanasifiwa na vyombo vya habari kwa mitazamo yao juu ya ugonjwa huo pamoja na hatua walizozianzisha kukabiliana na janga hili la afya.
Makala ya hivi karibuni katika jarida la Forbes liliwaonesha kama mfano wa kuigwa katika uongozi.
"Wanawake wamejitokeza na kuonyesha dunia vile wanavyoweza kuwa kupambana na kile ambcho kimejitokeza kuandama familia zetu", jariba la Forbes liliandika.
Wachambuzi nao wakiongeza kuwa wale wanaopita mtihani huu wa Covid-19 kwa kiasi kikubwa ni wanawake licha ya kwamba wale walio katika ngazi ya uongozi kama wakuu wa nchi kote duniani ni asilimia 7 pekee.
Je ni kipi kinachofanya viongozi wanawake kufanikiwa katika kukabiliana na janga la corona?

Waziri Mkuu wa Iceland Katrín Jakobsdóttir amegeukia upimaji wa virusi vya corona wa halaiki.Licha ya kwamba ni nchi yenye idadi ndogo ya watu ya 360,00, imekataa kulegeza kamba katika hatua za kupambana na Covid-19 kama vile kupiga marufuku mikusanyiko ya watu zaidi ya 20 au zaidi iliyochukuliwa mwishoni mwa Januari, kabla hata haijarekodi hata kisa kimoja cha ugonjwa huo.
Kufikia Aprili 20, watu 9 walikuwa wamekufa kwasababu ya Covid-19.
Huko Taiwan, ambayo ni sehemu ya China, Rais Tsai Ing-wen alianzisha kituo cha kudhibiti janga hilo na kuchukua hatua za kudhiiti na kufuatiliana wale walioambukizwa.
Taiwan pia mara moja ilianza uzalishaji wa vifaa vyake vya kujilinda kama vile barakoa. Hadi kufikia sasa imerekodi vifo 6 pekee miongoni mwa raia milioni 24 wa nchi hiyo.
Wakati huohuo, New Zealand, Waziri Mkuu Jacinda Ardern amechukua moja ya hatua kali zaidi ya kukabiliana na Covid-19. Badala ya kupunguza idadi ya visa vya maambukizi,kama vile ilivyodhihirika kwa nchi zingine, mbinu aliyotumia Bi. Ardern ni ya kuangamiza maambukizi yote.

Nchini humo kulitangazwa amri ya kusalia ndani vifo vilipofikia 6 pekee na kufikia Aprili 20, kwa ujumla vilikuwa vimefikia 12.
Lakini mbali na kwamba wanawake wanafanya vizuri katika kupambana na covi-19, nchi hizi ambazo zinachukuliwa kuendelea vizuri, zina wengine yanayofanana:
Hizi zote ni nci zenye uchumi ulioendelea, na mfumo wa ustawi wa jamii na mara nyingi huwa imeimarika kwa maendeleo ya jamii.
Kama iayojitikeza ni nchi zenye mifumo iliyoimarika ya afya yenye uwezo wa kukabiliana na hali ya dharura.
Kwahiyo, hilo linahusu viongozi wenyewe - au pengine pia inaangazia vile inavyomaanisha kuwa na kiongozi mwanamke katika nchi?
Kulingana na waangalizi, vile wanawake hao wanavyojitokeza na kufanya kampeni zao pia ni jambo la msingi.
"Sidhani kwamba wanawake mtindo mmoja wa uongozi ambao ni tofauti na wanaume. Lakini wanawake wanapokuwa katika nafasi za uongozi, hilo linachangia mbinu tofauti katika ufanyaji wa mamuuzi," amesema Daktari Geeta Rao Gupta, mkurugenzi wa Programu ya 3D kwa wasichana na wanawake na maafisa waandamizi katika wakfu wa Umoja wa Mataifa.
"Kunafanya kuwe na maamuzi mazuri kwasababu una maoni ya wanaume na wanawake," ameiambia BBC.
Ni tofauti kabisa na wale walioegemea siasa kwa baadhi ya viongozi wanaume kama Rais wa Marekani na Donald Trump na Brazil Jair Bolsonaro.
Rosie Campbell, mkurugenzi wa Taasisi ya Wanawake duniani katika chuo kikuu cha Uongozi wa wanawake cha King's London, anakiri kuwa mtindo wa uongozi sio sawa kwa wanaume na wanawake.
"Lakini kwa namna tunavyojadiliana, inakubalika kwa wanawake kuwa wenye huruma na ushirikiano zaidi. Na pia kuwa wanaume zaidi ambao pia wapo kwenye kundi hili watu binafsi, na ushindani wa kupitiliza", Campbell amesema.
Anaamini kuwa sifa kama hizo kwenye uongozi wa wanaume matatizo kwa misingi ya kisiasa".

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.