Habari za Punde

SAO HILL: MAZIWA YA NYUKI YA KINGA YA BINAADAM KUZEEKA


Mhifadhi wa shamba la Miti la Sao Hill kitengo cha Nyuki Wilayani Mufindi Said Abubakari moja kati ya mazao ya Nyuki katika shamba la miti la serikali ao Hill
Wavunaji wa mazo ya Nyuki katika shambva la miti la miti sao Hill Wilayani Mufindi
Baadhi ya waandishi mkoani Iringa wakifuatia zoezi la ufunaji wa mazao ya mdudu Nyuki 

Na.Fredy Mgunda - Mufindi.
WAKALA wa huduma za misitu Tanzania TFS kupitia shamba la miti la Sao hill Mkoani Iringa wanatarajia kuanzisha Mpango maalumu wa uvunaji wa sumu na maziwa ya nyuki yanayotajwa na watafiti wa masuala ya afya za binaadam kuwa na manufaa makubwa kiafya na fursa muhimu kiuchumi kupitia mazao yatokanayo na nyuki.

Mhifadhi wa shamba la Miti la Sao Hill kitengo cha Nyuki Wilayani Mufindi Said Abubakari Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Nyuki Duniani kwa upande wa mkoa wa Iringa na maeneo yaliyo chini ya wakala wa misitu Tanzania kupitia shamba hilo alisema mazao hayo yatachangia kuongeza pato la maduhuri ya serikali na ukuaji wa pato la wananchi wagao nyuki kutokana na mazao hayo kuhitajika zaidi katika matumizi ya mwili wa binadamu.
Alisema Maziwa ya nyuki pamoja na sumu inayozalishwa na Nyuki ni fursa muhimu kiuchumi katika soko la mazao yazalishwayo na wadudu hao huku akitanabaisha kuwa tafiti zinaeleza kuwa Maziwa ya nyuki yana Protini ya kiwango cha juu zaidi kuliko inayopatikana katika vyakula vingine na usaidia watu wanayoyatumia kutozeeka haraka, huku akiitaja sumu ya nyuki kuwa tiba muhimu ya binadam hasa kuhusu maradhi yanayohusisha tatizo la uvimbe kwa akina mama.

Abubakari alisema kwa mujibu wa tafiti mbalimbali sumu ya Nyuki inasaidia kutibu watu wenye uvimbe hasa hasa wanawake waliotoka kujifugua,ukipata dawa vizuri kwa mujibu ya wataalam uvimbe hupungua kila uchwao kutoka na dawa hiyo kufanya kazi kwa haraka.

“Uvimbe huo huanza kupungua taratibu kutoka matumizi bora ya dawa hiyo, Tupo katika hatua za awali za utafiti kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali na tukianza uzalishaji huo utakuwa na faida kubwa kwa wananchi wa Tanzania na nje ya Tanzania kwa kuwa hadi hivi sasa uvunaji wa sumu ya mdudu Nyuki inafanyika Tabora tu na sisi hapa tutafaata hivi punde” alisema Abubakari

Aidha Abubakari alisema Mpango wa SAO HILL ni kuwawezesha wafugaji Nyuki kupata mafunzo maalum ya uzalishaji wa maziwa kupitia malikia ambaye huzaa Nyuki wadogo ambao ndio hasa huzalisha zao la maziwa ya mdudu huyo.

“Maziwa ya mdudu nyuki huzalishwa na Nyuki wadogo ambao wanakuwa wamezalishwa kwa siku moja hadi siku mbili ndio ambao hasa ndio huwa wanakuwa na uwezo wa kuzalisha maziwa hayo” alisema Abubakari

Alisema kuwa pamoja na fursa hiyo kuwapo kwa wafugaji wa nyuki wanapaswa kutambua kuwa ulizalishaji wake unahitaji gharama kiasi huku na uhifadhi wa maziwa ya nyuki ukiwalazimu kuwa na vifaa maalum ambavyo vitawasaidia kuhifadhi maziwa hayo yatakayokuwa yamezalishwa na nyuki wadogo.

Akisisitiza kuhusu umuhimu wa maziwa ya nyuki Abubakari alisema kuwa maziwa ya hayo ni chakula ambacho kinaprotini isiyopatikana kwenye aina yeyote ya  Maharage au Nyama, na zao hilo utumiwa zaidi katika nchi zilizoendelea kutokana na umuhimu wake hasa juu ya virutumisho vinavyowasaidia watumiaji kutozeeka haraka kutokana kutokana na utumiaji wa virutubishi vilivyomo katika maziwa hao.

Abubakari aliongeza kuwa kando ya mazao ya hayo nyuki wamekuwa na manufaa makubwa kutokana na uchevushaji wanauofanya katika mimea mbali mbali huku akibainisha kuwa asali ni muongoni mwa mazao muhimu kwa afya ya binaadam ambayo katika maeneo mbalimbali ulimwenguni imekuwa ikitumika huku akiwataka wafugaji nyuki kuzingatia ubora ili kuiongezea thamani ili koboresha soko lenye kuaminika katika zao hilo.

Nao baadhi ya wafugaji wa Nyuki walisema kuwa wamekuwa wakipata faida kubwa kutokana na mazao wanayovuna kutokana na Nyuki hasa kupitiaa zao la Asali baada ya kupatiwa mafunzo kupitia wataalam wa shamaba la miti la Srikali la SAO HILL hatua iliyowawezesha kuzalisha mazao bora ya nyuki na kuwaongezea soko la uhakika ndani na nje ya nchi.

“Tumepata fursa ya kufuga Nyuki na tunawashukuru wenzet wa shamba la miti la Serikali SAO HILL kwa kweli kwa elimu waliyotupatia kwa kushirikiana na wakala wa Misitu Tanzania TFS imetusaidia sana kukuza vipato vyetu na mpaka sasa miongoni mwetu imekuwa ni ajira rasmi inayokidhi mahitaji yote muhimu” walisema.

Ikumbukwe Kupitia lengo namba moja la kutokomeza umasikini lililomo kwenye ajenda ya  maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa  ya mwaka 2030, serikali zinahimizwa kutafuta mbinu mbadala kuwawezesha wananchi kupitia miradi mbalimbali ili kujikwamua na umasikini ifikikapo mwaka 2030.

Lengo hili linakwenda sambamba na mikakati ya Shamba la miti la Serikali SAO HILLl katika kuendeleza shughuli za ufugaji wa nyuki na kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na nyuki

Kwa mujibu wa taarifa ya mwaka jana ya shirika la chakula ulimwenguni FAO asilimia 75 ya matunda na mbogamboga visingekuwepo bila nyuki na ni bidhaa ambazo ni muhimu sana kwa uhakika wa chakula na bayoanuai ya dunia.

Maadhimisho ya kimataifa ya siku ya nyuki duniani yalipitishwa rasmi na Baraza Kuu la Umoja wa mwaka 2017 na sasa yanaadhimishwa ulimwenguni kote kila ifikapo Mei 20 kila mwaka

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.