Habari za Punde

Wilaya ya Magharibi "B" Unguja Watakiwa Kubuni Vyanzo Vipya ya Mapato.

Na.Takdir Suweid Zanzibar.        
Sekta zilizogatuliwa zimeshauriwa kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuacha kutegemea vya zamani pekee.
Ushauri huo umetolewa na Makamo Mwenyekiti wa Kamati ya huduma za Jamii Thuwaiba Jeni Pandu wakati kamati hiyo ilipokutana na Sekta zilizogatuliwa ili kujadili matatizo na fursa mpya zilizopo za upatikanaji wa mapato katika Baraza hilo.
Amesema Serikali imefanya Ugatuzi katika Sekta ya Elimu, Afya na Kilimo ili kutoa huduma bora na rahisi kwa Wananchi.
Aidha amesema iwapo Shamba Darasa la ufugaji wa Kisasa litaimarishwa, Madiko na ushukaji wa Ngombe katika machinjio ya Kisakasa, Baraza hilo litaweza kukusanya Mapato kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande wao Viongozi wa sekta zilizogatuliwa katika Baraza la Manispaa Wilaya ya Magharibi ‘’B’’ wamesema wanakabiliwa na Tatizo la Idadi kubwa ya Wagonjwa wanaopkwenda katika baadhi ya Vituo vya Afya,Ukosefu wa hati Miliki na Idadi ndogo ya Wataalamu wa Mfumo wa kisasa wa Umwagiliaji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.