Habari za Punde

Watu 24 wapatikana na maambukizi ya corona kwa siku moja Kenya

Katibu mkuu katika Wizara ya Afya nchini Kenya Mercy Mwangangi amesema watu hao wamepatikana na Covid-19 kufuatia upimaji wa sampuli 1,195 katika kipindi cha saa 24.
Kenya imerekodi idadi kubwa ya maambukizi ya corona kwa siku moja , kuwahi kushuhudiwa tangu kisa cha kwanza cha maambukizi hayo kilipotangazwa tarehe 12 Machi
Akitangaza upatikana kwa visa vipya 24 vya maambukizi ya corona Katibu mkuu katika Wizara ya Afya nchini Kenya Mercy Mwangangi amesema watu hao wamepatikana na Covid-19 kufuatia upimaji wa sampuli 1,195 katika kipindi cha saa 24.
Dokta Mwangangi amesema kuwa saba kati ya visa hivi vipya vilipatikana katika kitongoji cha jiji la Nairobi cha Kawangware kinachokaliwa na idadi kubwa ya watu. Idadi ya visa vipya vya maambukizi iliyopatikana kwa ujumla jijini Nairobi imefikia 20.
Amesema 10 kati ya visa vipya vimepatikana katika eneo la Eastleigh jijini Nairobi huku watano wakitoka Mombasa na wawili kutoka Kuria West katika kaunti ya Migori.
Katibu huyo Mkuu wa Wizara ya Afria ametangaza pia kwamba mtu mmoja zaidi amekufa kutokana na virusi hivyo , na hivyo kuifanya jumla ya idadi ya vifo vya corona Kenya kufikia watu 22.
Wizara hiyo pia imeripoti kuwa watu wawili zaidi wameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kukutwa bila virusi, na hivyo kuongeza idadi ya watu waliopona kufikia 152.
Baadhi ya hatua zilizotangazwa na rais Uhuru Kenyatta za kukabiliana na janga la corona.
Chanzo cha Habari BBC News.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.