Habari za Punde

DKT. KIGWANGALLA AELEZA MAFANIKIO YA CCM JIMBO LA NZEGA VIJIJINI.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mlezi wa CCM mkoa wa Tabora, Ndugu, Afadhali Taib Afadhali akikabidhi pikipiki aina ya Boxer kwa Mwenyekiti wa CCM Kata ya Ugembe jimbo la Nzega vijijini. Pikipiki hiyo ni miongoni mwa pikipiki 40 zilizotolewa na Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ikiwa ni mchango wake wa kusaidia utendaji wa shughuli za Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye Kata na matawi mbalimbali ya jimbo hilo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mlezi wa CCM mkoa wa Tabora, Ndugu Afadhali Taib Afadhali akikabidhi baiskeli kwa viongozi wa matawi ya CCM jimbo la Nzega vijijini. Baiskeli 736 zimetolewa na Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini na Waziri wa Maliasili na Utalii,  Dkt. Hamisi Kigwangalla ikiwa ni mchango wake wa kusaidia utendaji wa shughuli za Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye Kata na matawi mbalimbali ya jimbo hilo.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Ndugu Hassan Wakasuvi akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya Chama cha Mapinduzi alipokua akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM jimbo la Nzega Vijijini.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mlezi wa CCM mkoa wa Tabora, Ndugu, Afadhali Taib Afadhali akizugumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM jimbo la Nzega vijijini .
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wa Jimbo la Nzega Vijijini wakifuatilia hotuba ya utekelzaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha miaka  iliyokuwa ikitolewa na Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini na Waziri wa Maliasili na Utalii,  Dkt. Hamisi Kigwangalla.
Sehemu ya pikipiki 40 na Baiskeli 736 zilizotolewa na Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini na Waziri wa Maliasili na Utalii,  Dkt. Hamisi Kigwangalla kwa Chama Cha Mapiduzi ikiwa ni mchango wake wa kusaidia utendaji wa shughuli za Chama hicho kwenye Kata na matawi mbalimbali ya jimbo hilo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mlezi wa CCM mkoa wa Tabora, Ndugu, Afadhali Taib Afadhali akizugumza jambo na Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini na Waziri wa Maliasili na Utalii,  Dkt. Hamisi Kigwangalla ikiwa mara baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa jimbo la Nzega vijijini.
PICHA/ Aron Msigwa – NZEGA.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.