Habari za Punde

Kada wa 20 CCM Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed Achukua Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar.

Kada wa Chama Cha Mapinduzi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammeed Aboud Mohammed akikabidhiwa Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar na Katibu wa Idara ya Oganizesheni ya CCM Zanzibar Ndg. Galos Nyimbo, hafla hiyo imefanyika katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar, akiwa Mwanacha wa 20 wa CCM kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Urais wa Zanzibar Octoba 2020.
Katibu wa Idara ya Oganizesheni ya CCM Zanzibar Ndg Galos Nyimbo akimkabidhi kitabu cha Ilani ya uchanguzi mgombea Urais wa Zabzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed wakati alipofika katika Afisi za CCM Kisiwandui kuchukua fomu ya kogembea kuteuliwa na Chama chake kugombea Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar Octoba 2020.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammede Aboud Mohammed akindika Kitabu Maalum cha Wagombea Urais wa Zanzibar wakati wa zoezi la kuchukua fomu ya Urais Afiki Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar. Akiandika namba za Kadi yake ya Uanachama wa CCM katika zoezi hilo la uchukuajhi wa fomu.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi Mgombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia CCM Mhe.Mohammed Aboud Mohammed akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu UWT Zanzibar Bi. Tunu Kondo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.