Habari za Punde

Kikao cha utoaji elimu ya kukabiliana na kukabiliana na maafa


Wajumbe wa Kamati Wilaya ya Kaskazini B wakimsikiliza  Mwenyekiti wa kamati ya Kukabiliana na Maafa Wilaya ya Kaskazini B,ambae pia ni  Mkuu wa Wilaya ya  Kaskazini B, Rajabu Ali  Rajabu huko katika ukumbi wa Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Mahonda ..
PICHA NA KHADIJA KHAMIS MAELEZO ZANZIBAR .
Mwenyekiti wa kamati ya kukabiliana na Maafa Wilaya ya kaskazini B ambae pia ni .Mkuu wa Wilaya ya  Kaskazini B, Rajabu Ali  Rajabu akifungua mkutano wa utoaji wa elimu wa zoezi la mezani kwa wajumbe wa kamati za wilaya  ya kukabiliana na maafa (katikati,) ( kulia) ni Ofisa Operesheni  kutoka Kamisheni ya  Kukabiliana na Maafa Shaaban Hasan na Mkurugenzi wa operesheni kutoka kamisheni wa kukabiliana na maafa Haji Faki Hamdani. huko katika ukumbi wa Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Mahonda .

Na Khadija Khamis- Maelezo       16/06/20202

Mwenyekiti wa Kamati ya Kukabiliana na  Maafa Wilaya ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B .Rajab Ali Rajab amewataka  Wajumbe wa kamati za wilaya zinazokabiliana na maafa kujenga mashirikiano ya pamoja ili kuzitatua changamoto za majanga kwa haraka  na ufanisi mkubwa .

Akiyasema hayo huko katika Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini, Mahonda wakati  akifungua mafunzo ya  utoaji wa elimu ya zoezi la mezani kwa wajumbe wa kamati ya kukabiliana na maafa wilaya yaliyoandaliwa na Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa.

Alisema  mashirikiano ya kiutendaji yatasaidia utatuzi wa haraka katika matukio ya maafa pamoja na utekelezaji wa majukumu kwa  mipaka  ya kiutendaji  kwa kila sekta  husika bila kuingilia majukumu ya wengine  .

Alifahamisha kuwa utendaji wa kazi kwa mpango shirikishi utasaidia mrejesho wa hali kwa haraka mara tu baada ya tukio kutokezea na  kuweza kuwafariji  kwa wakati wahanga waliopatwa na maafa .

“Kamisheni ya kukabiliana na maafa mjipange vizuri kwa kushirikiana na Kamati za Wilaya kuweza kuwafariji watu mara tu baada ya maafa sio kukaa mpaka wahanga wanasahau “alisema Mwenyekiti Rajab.

Hata hivyo  alisema kuwa tayari Serikali imesharuhusu ndege za kigeni kuingia nchini, kamisheni  ya kukabiliana na Maafa uweze kulifanyia kazi kwa haraka  daraja  la upenja njia inayoelekea kiwengwa kupitia kwenye mamlaka husika  ili kuepusha usumbufu kwa Watalii.

 Nae Mkurugenzi wa Operesheni kutoka Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Haji Hamdani amewataka wajumbe wa kamati ya maafa wilaya kutekeleza mpango wa zoezi la mezani ili kupunguza athari za maafa na dharura kwa jamii .

Alieleza kuwa kujitayarisha na maafa au majanga kutasaidia kujikinga kupunguza na kurejesha hali kwa haraka baada ya maafa kutokea .

Mkurugenzi huyo alisema kuwepo na utaratibu wa kijiografia katika wilaya kuweza kujua miezi ambayo majanga yalitokea au yanaweza kutokea kwa kujiandaa na  kujitayarisha,kwa kipindi cha majira tofauti.

 “Ili mpango wa kukabiliana na maafa wa Wilaya  uweze kufanya kazi zake kwa ufanisi litekelezwe chimbuko la lengo kuu la mpango kwa kufanyika zoezi la mezani  kwa wajumbe kuweza kujiweka tayari kupokea tukio kila wakati na kupokea taarifa pamoja na kuwepo vikao kwa kila robo mwaka vya kutathmini utekelezaji wa majukumu yenu “alisema Mkurugenzi Operesheni .

Hata hivyo Mkurugenzi huyo alisema zoezi la mezani litasaidi kujenga uwezo wa kiutendaji na kutatua tatizo kwa haraka kwa mujibu wa majukumu .

Nao wajumbe hao wameridhishwa na mafunzo hayo na kuwashukuru wakufunzi kutoka kamisheni ya kukabiliana na maafa na kuahidi mafunzo waliyoyapata watayafanyia kazi ili kuweza kufikia malengo ya kupunguza athari za maafa .

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.