Habari za Punde

WAKAGUZI WA MAZINGIRA DODMA WAPATIWA MAFUNZO

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Joseph Sokoine akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Wakaguzi wa Mazingira wateule Kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa zilizopo jijini Dodoma ambao watakuwa na jukumu la Kusimamia kikamilifu uzingatiaji na utekelezaji wa Sheria ya Mazingira yanayofanyika jijini Dodoma. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) yanatarajiwa kufungwa Ijumaa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamuwa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mussa Azzan Zungu.  
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Maduka Kessy akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kwa Wakaguzi wa Mazingira wateule Kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa zilizopo jijini Dodoma ambao watakuwa na jukumu la Kusimamia kikamilifu uzingatiaji na utekelezaji wa Sheria ya Mazingira yanayofanyika jijini Dodoma.
Washiriki wa mafunzo kwa Wakaguzi wa Mazingira wateule Kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa zilizopo jijini Dodoma wakiwa katika mafunzo ya kuwajengea uwezo katika kusimamia kikamilifu uzingatiaji na utekelezaji wa Sheria ya Mazingira yanayofanyika jijini Dodoma.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.