Na Jaala Makame Haji-ZEC
Tume
ya Uchaguzi ya Zanzibar itawapatia vitambulisho vipya vya kupigia kura Wapiga Kura
wote walioandikishwa na kuhakikiwa taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura ambavyo vitawawezesha kushiriki kupiga katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC THABIT IDAROUS FAINA alitoa kauli
hiyo baada ya kutembelea vituo vya Uandikishaji vya Wilaya ya Mjini kwa lengo
la kuangalia mwenendo wa utoaji huduma kwa wananchi wanaofika vituoni kwa ajili
ya kuandikishwa na kuhakikiwa taarifa zao.
Mkurugenzi
FAINA alisema kukamilika kwa zoezi la uandikishaji kwa mara ya pili ni hatua
ambayo itaifanya Tume kuweka wazi Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kabla ya
ugawaji wa Vitambulisho vipya vya kupigia Kura.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi alisema Tume imepata
mafanikio makubwa ya kukamilisha zoezi la uandikishaji kutoka na ushirikiano
walioupata kutoka kwa vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa vyama vya siasa
na Serikali pamoja na wananchi wote wa Zanzibar kuwa tayari na kushiriki katika
zoezi hilo.
Nao
wananchi waliofika katika vituo vya uandikishaji waliipongeza Tume ya Uchaguzi
ya Zanzibar kwa kuweka utaratibu mzuri
wa uandikishaji katika vituo vya uandikishaji na kuwaomba viongozi wa
Tume hiyo kuendelea kuwawekea mazingira mazuri katika hatua zote za uchaguzi ili uchaguzi huo ufanyike kwa uhuru na uwazi.
Wananchi
hao waliomba Tume kuendelea kuwaandalia mazingira mazuri ambayo yatawawezesha
kushiriki katika uchaguzi Mkuu bila usumbufu wowote na kuwataka wananchi wenzao
kutodharau fursa wanazopatiwa na viongozi wao katika majimbo ya Uchaguzi.
Kazi ya
Uandikishaji na uhakiki wa taarifa za Wapiga Kura kwa mara ya pili iliyofanyika
kwa kuwapa fursa ya kuandikishwa na kuhakikiwa taarifa zao wananchi waliokosa
huduma hizo kwa mara ya kwanza imeanza tarehe 30/5/2020 katika Mkoa wa Kaskazini
Pemba na imekamilika leo tarehe 12/6/2020 katika Wilaya ya Mjini.
No comments:
Post a Comment