Habari za Punde

Kasi ya Makada wa CCM Uchukuaji wa Fomu Ubunge CCM Kagera Yashika Kasi Biharamulo Wafikia 40

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM  Wilaya ya Biharamulo Bi. Adia Rashid Mamu Kulia akimkabidhi fumu ya kugombea ubunge Bw.Idrissa Songoro kushoto akiwa amefika ofisi hapo kuchukua fomu na kuingia kwenye idadi ya watia nia 40 wa wilaya hiyo hadi leo julai 15, mwaka huu.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM  Wilaya ya Biharamulo Bi. Adia Rashid Mamu kushoto akikagua kwa umakini  fomu za mgombea ubunge jimbo la Biharamulo Mhandisi Ezra Chiwelesa baada ya kurejesha fomu hizo ofisini kwake.
Eng.Ezra Chiwelesa Kushoto mgombea ubunge jimbo la Biharamuro CCM akimkabidhi Fomu Katibu wa CCM Wilaya ya Biharamulo Bi Adia Rashid Mamu Kulia baada ya kuichukua fomu hiyo julai 14 mwaka huu dirisha la uchukuaji fomu lilipofunguliwa rasmi na kuirejesha leo julai 15,mwaka huu akiwa ameijaza.
Na Allawi Kaboyo Biharamulo.
Ikiwa ni siku ya pili ya kuchukua na kurejesha fomu za kugombea ubunge na udiwani kwa wanachama wa chama cha mapinduzi kote nchini, waliochukua fomu za kugombea ubunge wa jimbo la Biharamulo sasa wafikia 40 ambapo 7 kati ya hao ni wanawake.
Hayo yamebainisha leo na Bi Adia Rashid Mamu katibu wa ccm wilaya ya Biharamulo alipokuwa akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake kwa lengo la kueleza mwenendo mzima wa uchuaji fomu unavyoenedelea wilayani humo.
Bi Adia ameeleza kuwa wananchama katika wilaya hiyo wamehamasika na kujitokeza kutekeleza haki yao ya kikatiba kama wananchama na kuongeza kuwa hamasa hiyo inatokana na mambo makubwa yaliyofanywa na serikali ambayo ipo chini ya chama chao ikiongozwa na Rais Magufuli.
Amesema kuwa uchukuaji wa fomu za ubunge umegusa rika zote huku akionyesha kufurahishwa na wingi wa wananwake waliojitokeza kugombea jimbo hilo pamoja na vijana na kuwataka watia nia hao kufuata kanuni na taratibu za chama na kuongeza kuwa licha ya idadi hiyo kuwa kubwa mbunge aliyemaliza muda wake bado hajajitokeza kuchukua fomu.
“Mwenendo wa uchukuaji fomu za ugombea hapa kwetu unakwenda vizuri na wanachama wamehamasika kwa wingi kuchukua fomu, kinachonifurahisha Zaidi ni kuona wanawake na vijana wamejitokeza hili linaashiria kuwa ndani ya chama chetu demokrasia imetawala na kuonyesha uongozi sio wa watu Fulani. Niwaombe wananchama waendelee kujitokeza kuja kuchukua fomu maana fomu zipo na gharama yake ni shilingi laki moja ambapo mgombea anaweza pia kutoa mchango wa hiari kwaajili ya kuchangia chama katika mchakato mzima wa kampeni.” Amesema Bi Adia
Aidha katibu huyo amesema kuwa maandalizi kuelekea kwenye kura za maoni yapo vizuri ambapo amebainisha kuwa katika wilaya hiyo wapo Zaidi ya wajumbe 600 ambao wote wanatarajia kushiriki kikamilifu uchaguzi huo ndani ya Chama na hatimaye wakampata mgombea atakayepeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba mwaka huu.
Nje ya ofisi hiyo walikuwepo baadhi ya watia nia ambao walikuwa wananendelea kuchukua fomu na wengine wakirudisha fomu ambao miongoni mwa wagombea hao ni Mhandisi Ezra Chiwelesa ambaye amefika ofisini hapo kurejesha fomu na kuwaeleza waandishi wa habari kuwa yeye kama kijana ameamua kugombea ubunge ili kuwatumikia wanabiharamulo.
Ezra ameongeza kuwa mfumo uliopo ndani ya chama chao unaweka uhuru wa kila mwananchama kugombea hivyo ameamua kuja Biharamulo kuweza kukabiri baadhi ya changamoto ambazo kwazo zimekuwa kero ya muda murefu kwa wananchi wa wilayao hiyo.
“Nimeamua kuchukua fomu ya kuomba kugombea nafasi ya ubunge kupitia chama change nikiamini mimi na weza kuwatumikia wananbiharamulo, chama chetu sasa ni kipya na mimi nataka Biharamulo yetu iwe mpya na iwe sehemu ya kuwavutia wawekezaji maana tayari tunayo mbuga inayopita kwenye wilaya yetu ya BURIGI CHATO hii ni fursa kwa wananchi wa Biharamulo.” Amesema Mhandisi Ezra.
Ameeleza kuwa katika mchakato wote anawasihi watia nia wenzake kutotumia Lugha chafu kwa wagombea wenza na kuwataka wajumbe kutojihusisha na vitendo vya rushwa kwa kushawishiwa na baadhi ya wagombea na kuwapa vijisenti ili wawachague huku wakijua wanatangeneza mstakabali wa maisha yao ya miaka mitano ijayo.
Mwingine aliyekuwepo ni Bw. Idrissa Songoro ambaye naye amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea ubunge wa jimbo hilo ambapo ameeleza kuwa kutokana na demoklasia iliyopo ndani ya chama anajiona anatosha kuwatumikia wananbiharamulo.
Katika wilaya ya Missenyi waliojitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Nkenge wafikia 46 hadi julai 15 mwaka huu ambapo miongoni mwa watia nia hao wamo waliowahi kuwa wabunge wa jimbo hilo ambao ni Balozi Dkt. Deodorus Kmara mbunge aliyemaliza Muda wake, Mhe.Asumputa Mshama aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa Katibu wa chama hicho wa wilaya Missenyi Emanuel Alex ameeleza kuwa miongoni mwa watia nia hao wane kati ya hao ni wananwake huku akizidi kuhamasish wananchama kwenda kuchukua fomu ili waweze kukipigania chama chao.
Aidha kwa upande wa Jimbo la Ngara watia nia waliochukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM wafikia 39 hadi julai 15 mwaka huu huku mmoja kati ya hao ni mwanamke.
Kwamujibu wa katibu wa ccm wilaya ya Ngara Mapanga Nelele amesema kuwa mwenendo wa uchukuaji fomu unakwenda vizuri ambapo ameeleza kuwa miongoni mwa watia nia hao yumo mbunge aliye maliza muda wake Mhe. Alex Gashaza ambaye nay eye amechukua fomu kwaajili ya kuitetea nafasi yake ambapo ameongeza kuwa waliochukua fomu kuwania udiwani viti maalumu wamefikia 16.
Nelele amewasihi wagombea kuendelea kufata kanuni na taratibu za chama katika mchakato mzima ili waweze kuenzi katiba ya chama chao na kuwasihi wanachama kuendelea kuzitumia siku zilizobakia kujitokeza kuchukua fomu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.