Habari za Punde

Mwenyekiti wa Chama cha ADC Mhe. Hamad Rashid Achukua Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar.

Mkurugenzi Mipango na  Uchaguzi wa Chama Cha ADC Taifa Ndg.Omar Albet Constantine akimkabidhi fomu ya kugombea Uraisi Mwenyekiti wa ADC Mhe. Hamad Rashid Mohammed (kulia mwenye kofia) hafla hiyo imefanyika katika Afisi za ADC Bububu Jijini Zanzibar.
Mtangaza nia kugombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ADC Mhe. Hamad Rashid Mohammeed akiwa na mkoba wa fomu za kugombea Urais wa Zanzibar baada ya kukabidhia Fomu za kugombea Urais na  Mkurugenzi Mipango na  Uchaguzi wa Chama cha ADC Taifa Ndg. Omar Albet Constantine.(hawapo pichani ) akiwaonesha Waandishi wa habari walioshuhudia hafla hiyo iliofanyika katika Ofisi za Chama hicho Bububu Jijini Zanzibar.
 Picha na Fauzia Mussa - MAELEZO.

Na Sabiha Khamis na Ali Issa – Maelezo    09/07/2020
Mwenyekiti wa chama cha (Alliance for Democratic Change) ADC Hamad Rashid Mohamed amesema iwapo wananchi wa Zanzibar watamchagua kuwa Rais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao ataimarisha sekta ya elimu na kutoa huduma hiyo bure hadi kufika kiwango cha elimu ya juu.
Hayo ameyasema katika ofisi yao huko Mtopepo Wilaya ya Magharibi “A” wakati alipokuwa akichukua fomu ya kuombea ya urais kupitia chama hicho amesema pindipo atapata madaraka ya kuongoza nchi  atahakikisha kuwa serikali yake inatoa huduma hiyo bila ya gharama yoyote kwa wananchi.
Amesema yeye  ni mzalendo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanibar hivyo atafanya juhudi hiyo na kuhakikisha kwamba jambo hilo linafanikiwa mara tu baada ya kuingia madarakani.
“Pindipo nitapata ridhaa ya kuchaguliwa kwa kura nyingi kuwa rais wa Zanzibar nitahakikisha kuwa wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu wanaochukua degree ya kwanza watasoma bure bila ya gharama yoyote kulipia katika mtaala huo wa elimu”, alisema Mhe. Hamad Rashid.
Aidha Mhe. Hamad alieleza kuwa pia ataimarisha ujenga nyumba za maendeleo zenye ghorofa tatu mpaka nne kila wilaya ili kuepuka migogoro ya ardhi pamoja na kuharibu mazingira.
Hata hivyo amefahamisha kuwa atainua uchumi wa Zanzibar kwa kupitia kilimo na uvuvi wa kisasa ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa hizo pamoja na kuwaunganisha walimu wa madrasa na serikali pamoja kutoa hati ya kusafiria, kitambulisho cha Mzanzibar na Uraia wa nchi mbili kwa lengo la kuleta maendeleo .
 Nae Mkurugenzi Mipango Uchaguzi wa chama hicho Omar Albat Costatine amesema fursa ya ugombea Urais wa chama chao ipo wazi kwa yoyote yule mwanachama muhimu kuzingatia sheria ya chama na miongozo iliopo.
Aidha alisema mgombea yoyote yule anae chukua fomu ya urais kupitia chama hicho atalazimika kuwa na wadhamini 100 kwa kila mkoa .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.