Habari za Punde

MKURUGENZI ZSSF AFURAHISHWA NA USHIRIKIANO KATI YA PSSSF NA NSSF MAONESHO YA SABASABA 2020.



MKURUGENZI Mwendeshaji wa FUKO wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Bi. Sabra Issa Machano amefurahishwa na namna mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na ule wa NSSF kutumia banda moja katika maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaa wakati alipotembelea banda hilo Julai 7, 2020.

“Nimefurahi sana kufika hapa leo katika banda la pamoja la PSSSF na NSSF tayari Mfuko wetu unaushirikiano na NSSF tutaangalia namna tunavyoweza kushirikiana na PSSSF ili tuweze kuondoa changamoto zinazowakabili wafanyakazi wanaohama kutoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar au Zanzibar kuja Bara.” A;lisema Bi. Sabra.

“Kuhama kwa wafanyakazi kutoka sehemu moja ya Tanzania iwe bara au Zanzibar kumepelekea changamoto ya kuwahudumia wafanyaakzi hao hususan katika suala la michango katika mifuko mitatu ya hifadhi ya Jamii yaani ZSSF ya Zanzibar kwa upande mmoja na PSSSF na NSSF kwa upande wa Tanzania bara.” Alisema Mkurugenzi huyo na kuongeza…..Changamoto kubwa inayoikabili mifuko hii mitatu kwa sasa ni movement ya wafanyakazi Tanzania 

Na kwa sasa hivi changamoto hii tumeiona hasa kwenye mahoteli, wafanyakazi wengi wa mahotelini wanatoka Tanzania bara wanakuwa wanatamani kuhama wakati umefika sasa tuangalie kwa wale wafanyakazi wanaofanya kazi Zanzibar na wanatoka Tanzania bara au wale wanaofanya kazi Tanzania bara na wanatoka Zanzibar wakihamia sehemu moja ya Tanzania tutawahudumia vipi, swala hili ni muhimu tukaliangalia ili tulipatie ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.