Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wahamaji (IOM) Dkt. Qasim Sufi akimkabidhi Pikipiki Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Halima Maulid Salum katika hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja .
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Maulid Salum akitilIana saini na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wahamaji (IOM) Dkt.Qasim Sufi wakati wa makibidhiano ya msaada wa pikipiki hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja .
Baadhi ya Maafisa wa Wizara ya afya wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupokea msaada wa pikipiki kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wahamaji (IOM) hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja .
PICHA NA FAUZIA MUSSA/ MAELEZO
Na.Issa Mzee, Maelezo 09/07/2020
Wizara ya afya imepokea msaada wa pikipiki mbili zenye thamani ya dola 2727 kutoka shirika la Umoja wa Wataifa la kuhudumia Wahamaji (IOM) kwa lengo la kuwasaidia wafanyakazi kufuatilia maradhi ya Corona.
Akikabidhi msaada huo Mkuu wa Shirika la Wahamaji Tanzania Dkt. Qasim Sufi huko Wizara ya Afya Mnazimmoja, amesema lengo la msaada huo ni kuiwezesha na kuirahisishia serikali ya Zanzibar katika jitihada za kupamabana na maradhi hayo.
Aidha amesema shirika hilo litazidi kutoa ushirikiano katika sekta ya afya ili kupambana na maradhi mbalimbali ikiwemo ya kuambukiza .
Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Maulid Salum amesema pikipiki hizo zitawawezesha kufutilia mwenendo mzima wa maradhi .
Alisisitiza kwamba zitawasaidia katika kufanya tafiti za maradhi mbalimbali hasa maeneo ya ndani ambayo ni vigumu kufikika kwa kutumia usafiri wa gari .
“baadhi ya sehemu hasa vijijini inakua usumbufu kufika kwa gari, hivyo msaada huu utatusaidia kwa kiasi kikubwa ” alisema Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Nae Mkurugenzi kinga Dk Fadhil Mohamed amelishukuru shirika hilo kwa msaada huo na kuwataka wafanyakazi kuzitumia vizuri pikiki hizo ili kufikia malengo.
Amewataka watendaji waliokabidhiwa pikipiki hizo kuzitumia ipasavyo na kuzitunza ili ziweze kudumu
No comments:
Post a Comment