Habari za Punde

Wateja wa Zantel kununua tiketi za boti za Azam kwa Ezypesa.Ni baada ya Zantel kuingia ubia na Kampuni ya Kilimanjaro Fast Ferries, hatua itakayorahisisha upatikanaji wa huduma za usafiri.Zanzibar, Agosti 13, 2020. Wateja waZantel wataweza kununua tiketi za usafiri wa boti za Azam kwa njia ya Ezypesa baada ya kampuni hiyo kuingia ubia na Kampuni ya usafirishaji ya Kilimanjaro Fast Ferries Ltd inayotoa huduma za usafiri wa boti.

Kampuni hiyo ni moja ya watoa huduma za usafiri wa majini kati ya Zanzibar na Dar es Salaam ikiwa na boti nne zinazochangia katika urahisishaji wa huduma za usafiri kwa wenyeji na wageni.

Akizungumzia hatua hiyo, Mkuu wa Masoko na Huduma za Kifedha wa Zantel, Sakyi Opoku alisema hatua hiyo imelenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za ukataji tiketi kwa abiria hivyo kuboreshamaisha ya wateja wao.

“Kwa kupitia Ezypesa tunahakikaisha wateja wanafanya malipo yao kwa urahisi zaidi,mahali popote na wakati wowote.Ushirikiano wetu na Kilimanjaro Fast Ferries unawapa wateja uhuru wa kununua tiketi na kupunguza muda na mchakato wa kununua tiketi,” alisema Opoku.

 Ili kupata huduma hiyo, mteja wa Zantel, atapiga namba ya Azam bure 0800 785 555 na atapewa namba ya kumbukumbu ya malipo.Kisha ataenda kwenye menyu ya Ezypesa *150*02#na kuendelea na malipo, kisha ingiza namba ya Kampuni777444 kisha kumbukumbu namba,kiasi na mwisho thibitisha malipo.

“Tunaamini njia hii ni suluhisho na itaboresha namna wateja wanavyopata huduma za usafiri hususan wasafiri wa ndani kwani kwa sasa hakuna haja ya kwenda tena katika ofisi bali ukiwa na simu yako tu unaweza kujihakikishai uhakika wa kupata usafiri,” alisema Opoku.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Marine Ltd, Abubakar Salim alisema kampuni hiyo imewekeza katika mifumo ya malipo mtandaoni ambayo inatumika duniani kote, ambayo imesaidia kuboresha upatikanaji wa huduma za usafiri.

“Ushirikiano baina yetu na Ezypesa umetanua wigo wa njia za malipo ambazo zinampa mteja uhuru wa kununua tiketi mahali popote alipo, wakati wowote bila malipo ya ziada,” alisema Salim.

Wateja watakaofanya malipo kwa Ezypesa watachukua tiketi zao katika ofisi za Azam Marine siku ya kusafiri ambapo watatakiwa kuonyesha ujumbe (SMS) ya uthibitisho wa malipo.

 Kuhusu Zantel

Zantel ni Kampuni inyaoongoza kwa utoaji wa huduma za mawasiliano Visiwani Zanzibar kwa miaka mingi hivi sasa ikiongoza kwa ubora miundombinu ya mawasiliano, huduma pamoja na bidhaa.

Huduma ya kifedha ya Ezypesa ni ya kwanza nchini Tanzania kutoa huduma za kibenki za kawaida pamoja na za kiislamu kwa ushirikiano na benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

Aidha, Zantel ni kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za intaneti nchini Tanzania kupitia uwekezaji kwenye teknolojia ya fibre optic cable ambayo inaiunganisha Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki na duniani umeiwezesha Kampuni hiyo kuleta mapinduzi ya haraka ya kidigitali hapa nchini.

Aidha,Miundombinu hiyo  imeiwezesha Zantel kutoa huduma za kimataifa za sauti na data kwa jumla kwa kampuni nyingine na nchi jirani hivyo kuchagiza ukuaji wa teknolojia ya digitali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.