Habari za Punde

Balozi Seif Atembea Ujenzi wa Makazi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Eneo la Mtaa wa Pagali Chakechake Pemba.

Muonekano wa Nyumba ya Makaazi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Kisiwani Pemba ukionyesha haiba nzuri ya kupendeza inayolingana na hadhi ya Kiongozi wa Kitaifa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa Pili kutoka Kulia akipatiwa maelezo ya maendeleo ya Ujenzi wa Nyumba ya Makaazi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Kisiwani Pemba kutoka kwa Mshauri Muelekezi wa Wakala wa Ujenzi Zanzibar aliyepo Kisiwani Pemba Mhandisi Said Malik Said wa kwanza Kutoka Kulia hapo Mtaa wa Pagali Chake chake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed akimuhakikishia Balozi Seif Ali Iddi ujenzi wa Mradi huo kumalizika wakati wowote kuanzia sasa baada ya kuwekwa samani za ndani.

Na.Othman Khamis.OMPR.

Ujenzi wa Nyumba ya Makaazi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika Mtaa wa Pagali Chake Chake Kisiwani Pemba uliolenga kuondosha tatizo la Makaazi kwa Mtendaji huyo Mkuu wa Serikali unatarajiwa kukamilika  wakati wowote kuanzia sasa.

Mshauri Muelekezi wa Ujenzi huo kutoka Wakala wa Ujenzi Zanzibar aliyepo Kisiwani Pemba Mhandisi Said Malik Said alisema ujenzi huo ulioanza Mnamo Mwaka 2018 tayari umeshafikia asilimia 97% umekisiwa kugharimu  jumla ya shilingi Bilioni Moja Nukta Sita {1,600,000,000/-} hadi kukamilika kwake.

Akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika Pagali kukagua  maendeleo yaliyofikiwa ya Ujenzi huo Mshauri Muelekezi Said Malik Said alisema hivi sasa wahandisi wa ujeni huo wanakamilika mkono wa mwisho wa rangi katika Majengo hayo.

Alisema miundombinu ya Huduma za Umeme, Vipoza Hewa, Maji, Bara bara  za ndani za Makaazi hayo imeshakmilika na kinachomaliziwa katika Mradi huo kwa hivi sasa ni ukamilishaji wa Bustani ili kuyapamba Makaazi hayo yanayohitajika kuwa na hadhi ya Kiongozi wa Kitaifa.

Mhandisi  Said alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba  licha ya mradi huo wa Ujenzi kuendelea kusimamiwa Kitaalamu lakini bado Ushauri wa Wataalamu wa Wakala wa Ujenzi utazingatia kufuatilia Mradi huo hadi pale watakapojiridhisha kwamba umekidhi vigezo vyote walivyoshauri na kuelekeza.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed Katibu Mkuu Nd. Shaaban Seif Mohamed pamoja na Watendaji wa Ofisi yake alielezea faraja na  kuridhika kwake na hatua iliyofikiwa ya Ujenzi wa Mradi huo.

Balozi Seif  ameonyesha shauku ya kutaka kuyatumia Makaazi hayo mara tu yatakapokamilika kabla ya kumaliza Utumishi wake wa Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar utakaofikia kikomo chake mara baada ya uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba Mwaka huu.

Miradi ya Ujenzi wa Majengo ya kudumu ya Ofisi za Serikali, Makaazi ya Viongozi na Nyumba za Kisasa kwa Wananchi ni muendelezo wa falsafa ya Chama cha Afro Shirazy Party chini ya Muasisi wake Marehemu Mzee Abeid Aman Karume ambayo imekuwa ikitekelezwa na Viongozi wa Awamu zote Saba za SMZ tokea Mapinduzi Matuufu ya Mwaka 1964.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.