Na Mwashungi Tahir Maelezo .
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wametakiwa kuwa watulivu kutokana na tukio lililotokea huko kisiwani Pemba la kupigwa mapanga watu watatu wakiwa katika sehemu ya kufanyia Ibada.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa Kamati maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Catherine Peter Nao kuhusiana na tukio hilo huko katika ukumbi wa Afisi ya Kiswandui na kulaani kwani ni tendo la kinyama na kusikitisha jamii.
Amesema nchi bado ina amani na kuwataka wanachama kuwa watulivu, kuondosha hofu kwani Jeshi la Polisi linafanya kazi yake na wahusika wanafuatiliwa ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Hata hivyo amesema lengo la kufanya vitendo hivyo ni kuwatia woga wanachama wa CCM huko Pemba ili ikifika siku ya kupiga kura waogope kufika vituoni na kuchagua viongozi wanaowataka.
“Kufanya hivyo ni kutaka kuwatia hofu ili muogope kwenda kupiga kura lakini ondosheni hofu na ikifika siku jitokezeni kwa wingi kwenye vituo vya kupiga kura kwani vyombo vya ulinzi vitaimarishwa zaidi”,alisema Catherine.
Aliwaomba wananchi wawe watulivu na Chama cha Mapinduzi kipo pamoja na waliofikwa na kadhiya hiyo,na kuwataka familia iwe na subra
Pia amesema CCM sio chama cha kulipiza kisasi mambo ambayo hayafai katika jamii kwani chama hicho hufuata miongozo iliopo ndani ya ilani na kinaongoza vizuri na kukubalika na jamii kuongoza dola.
No comments:
Post a Comment