Habari za Punde

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Mhe.Dk.Shein Amtambulisha Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Husseinn Mwinyi Viwanja Vya Gombani ya Kale Chakechake Pemba leo 16/9/2020.

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi Mhe Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi akiwasalimia Wanachama wa CCM wakati akiwasili katika Uwanja wa Gombani ya Kale Chakechake Pemba wakati wa Ufunguzi wa Mkotano wa Ufunguzi wa Kampeni za CCM Pemba. Ufunguzi huo umefanywa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(hayupo pichani) 
Rais Mstaaf wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa CCM Pemba wakati akiwasili katika Uwanja wa Gombani ya Kale Chakechake Pemba akiwa na Mkewe Mama Siti Mwinyi, wakihudhuria hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa Kampeni ya CCM Pemba.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Mwinyi, alipowasili katika Uwanja wa Gombani ya Kale Chakechake Pemba CCM kuhudhuria Ufunguzi wa Mkutano wa Kampeni wa CCM Pemba.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimtambulisha Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi katika Ufunguzi wa Mkutano wa Kampeni wa CCM Pemba uliofanyika katika Uwanja wa Gombani ya Kale Chakechake Pemba (kulia kwa Rais) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi na Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe,.Dk. Hussein Mwinyi.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi wakati wa mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni ya CCM Pemba iliofanyika katika Uwanja wa Gombani ya Kale Chakechake Pemba.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi Ilani ya  Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Hassan Mwinyi  katika Uwanja wa Gombani ya Kale Chakechake Pemba wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Kampeni ya CCM Pemba, kuwatambulisha Wagombea Ubunge, Uwawakilishi na Udiwani. 
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Mhe.Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi akiwaonesha Ilani ya Uchaguzi ya CCM WanaCCM baada ya kukabidhiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dk. Ali Mohamed Shein. wakati wa Ufunguzi wa Kampeni za CCM Pemba zilizofanyika Uwanja wa Gombani Chakechake. baada ya kutambulisha kwa WanaCCM Pemba

Mgombea Urais wa Zanzibar  kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi akiwahutubia Wananchi na WanaCCM katika wakati wa Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni ya CCM Pemba na kutambulishwa kwa Wananchi wa Pemba katika Uwanja wa Gombani ya Kale Chakechake Pemba.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Pemba wakifuatilia mkutano wa Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi uliofanyika katika Uwanja wa Gombani ya Kale Chakechake Pemba. 

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Pemba wakifuatilia mkutano wa Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi uliofanyika katika Uwanja wa Gombani ya Kale Chakechake Pemba. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.