Habari za Punde

Wateja wa Zantel kulipia bili za Maji kwa Ezypesa Zanzibar.

  

 

Hatua hiyo itaongeza urahisi wa malipo huku ikiongeza ufanisi wa mamlaka ya maji katika utoaji wa huduma.

Kwa sasa wateja wa Zantel wanaweza kuipia bili za maji kiurahisi zaidi kwa njia ya Ezypesa baada ya kampuni hiyo kuingia ubiana Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), mfumo wa kidigitali zaiid wa kufanya malipo.

Hatua hiyo itaongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato huku ikiwapunguazia wateja adha ya kusafiri umbali mrefu ili kulipia huduma hiyo muhimu.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Zawa, Mussa Ramadhan alipongeza hatua hiyo akieleza kuwa itasaida katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja visiwani Zanzibar.

“Mkakati wetu ni kuendeleza na kutoa huduma ya maji ya uhakika na nafuu kwa wateja wetu, hivyo ushirikiano wetu na Ezypesautasaidia katika kufikia malengo yetu kwani utaongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato na kuwapunguzia wateja mzigo wa kutembea umbali mrefu kwani kwa sadsa kila kitu kitafanyika kwa simu,” alisema.

Huduma hiyo ni suluhisho katika kuongeza kasi na ufanisi wa ukusanyaji wa mapato hivyo kusaidia mamlaka kuwa na uwezo wa kuboresha miundimbinu ya maji na kuwafikia watu wengi zaidi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Khamis Mussa alisema hatua hiyo ni muhimu katika kutekeleza mkakati wa Zantel wa kuboresha Maisha ya watu kupitia huduma za Ezypesa ambazo zinawapa wateja wake uhuru na urahisi wa kupata huduma mbalimbali.

“Kupitia Ezypesa tumejidhatiti katika kuboresha Maisha ya watu kwenye Nyanja mbalimbali ili kuwezesha urahisi wa upatikanaji wa huduma na mahitaji ya kila siku.Ushirikiano wetu na ZAWA ni hatua muhimu katika kuhakikisha wateja wetu wanalipia ankara za maji mahali popote,” alisema Mussa.

Aliongeza “Tofauti na njia za awali, kwa sasa hakuna haja tena ya kutembea umbali mrefu ili kulipia bili au usubiri mpaka maji yakatike kwa kuchelewesha bili, kwa simu yako tu unaweza kujihakikishai unapata huduma ya maji.”

Ni dhahiri kuwa maji ni rasilimali muhimu katika kuchochea huduma za kibiashara Pamoja na zile za majumbani.Mamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA) inafanya jitihada kubwa kusimamia huduma ambayo hadi sasa imewafikia wateja 1,161,915 visiwani Zanzibar.

Ili kulipa bili, mteja wa Zantel atapiga *150*02# kisha 5 Malipo na Kisha 7 Kisha chagua 3 Bili za Maji kisha ZAWA na endelea na malipo kwa kuingia namba ya akaunti ya maji iliyopo kwenye bili yako na kiasi kisha thibitisha. Mteja atapata ujumbe (SMS) kwa malipo yaliyofanyika.

 

Kuhusu Zantel

Zantel ni Kampuni inyaoongoza kwa utoaji wa huduma za mawasiliano Visiwani Zanzibar kwa miaka mingi hivi sasa ikiongoza kwa ubora miundombinu ya mawasiliano, huduma pamoja na bidhaa.

Huduma ya kifedha ya Ezypesa ni ya kwanza nchini Tanzania kutoa huduma za kibenki za kawaida pamoja na za kiislamu kwa ushirikiano na benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

Aidha, Zantel ni kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za intaneti nchini Tanzania kupitia uwekezaji kwenye teknolojia ya fibre optic cable ambayo inaiunganisha Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki na duniani umeiwezesha Kampuni hiyo kuleta mapinduzi ya haraka ya kidigitali hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.