Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar ZEC imezitaka Asasi za kiraia ambazo zimepewa vibali vya kutoa elimu ya wapiga kura kuzingatia zaidi matakwa ya
sera ya jinsi na ushirikishwaji wa makundi ya kijamii ya mwaka 2015
iliyoanzishwa na tume kwa lengo la kuyashirikisha kikamilifu makundi hayo katika masuala ya uchaguzi
Akifungua mkutano ambao umeshirikisha Asasi za kiraia,
makundi ya vijana na wanawake huko katika ukumbi wa kituo cha waandishi,
waangalizi na matukeo ya uchaguzi maruhubi, Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe. Jaji Mkuu (mst)
Hamid Mahmoud Hamid alisema Tume imewaamini na kuwapa vibali vya kutoa elimu kwa jamii ili waweze kushiriki kikamilifu katika masuala ya Uchaguzi.
Akiwasilisha mada kuhusu matayarisho ya uchaguzi mkuu 2020 Mkurugenzi wa uchaguzi Thabit Idarous Faina alieleza kuwa, bajeti na mpango kazi wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 uliandaliwa na kuwasilishwa Serikalini ambapo Serikali imeipatia Tume mahitaji yote ya bajeti iliyowasilishwa kukamilisha majukumu yake.
“hadi tunavyozungumza katika mkutano huu uagiziaji wa vifaa na huduma za Uchaguzi zimekamilika.
Karatasi za kura zinaendelea na hatua ya uchapishaji ambao unatarajiwa kukamilika wiki
mbili kabla ya siku ya uchaguzi ili ziweze kusambazwa kwa wakati” alisema.
Akizungumza kuhusu kura ya mapema Mkurugenzi Faina alisema tarehe
27 Oktoba, 2020 ZEC
itaendesha kura ya Mapema ambayo itahusisha watendaji wa Uchaguzi na walinzi wanaohusika na ulinzi na usalama siku ya Uchaguzi ili watu hao waweze kupiga kura ya mapema.
Hata hivyo,
Ndugu Faina alifafanua kuwa, Wapiga Kura wa Kura ya mapema wakiwemo wale
wanaohusika na ulinzi na usalama siku ya Uchaguzi ni lazima wawe wameandikishwa katika Daftari
la Kudumu la Wapiga Kura
Akizungumza kwa niaba ya mrajis wa asasi za kiraia Mwanabaraka Saleh Sheha amezitaka asasi kufuatu amaelekezo ya tume ambayo ni muhimu katika katanua wigo wa kuelimisha umma katika hatua zote za uchaguzi.
Nao washiriki wa mkutano wamewataka wananchi kutafakari na kufanya maamuzi sahihi katika kuchagua viongozi siku ya kupiga kura.
No comments:
Post a Comment