Habari za Punde

Kiwanda Cha Mkaa Gandamizi Njiani Kuwanufaisha Wananchi Mkoani Tanga na Taifa Kwa Jumla.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Tanzania Prof Riziki Shemdoe akiwa katika ziara yake kutembelea kiwanda cha Africa Flame Ltd kinachotarajiwa kuaza uzalishaji wa mkaa gandamizi hivi karibuni akipata maelezo kutoka kwa muhusika wakati wa ziara yake. 

Na Hamida Kamchalla, TANGA.                                                                                                                

KATIBU Mkuu wa wizara ya viwanda na biashara Prof. Riziki Shemdoe amesema ziara yake ya leo jijini Tanga ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa wizara hiyo kwa lengo la kutuhusu viwanda vimpya kufunguliwa.

Prof. Shemdoe ameyasema hayo leo akiwa kwenye kiwanda cha Africa Flame l.t.d kinachotarajia kuanzisha uzalishaji wa mkaa gandamizi unaotokana na maligafi za mazao ya miti hususani ya mbao na chakula aina ya mnazi.

"Maligafi zenu ni rafiki hata kwa mazingira, wale watakaofuata bidhaa hizi watakuwa wakitusafishia mazingira na kuziweka bichi zetu katia hali nzuri, kiwanda hiki kitatoa ajira kwa wananchi wa Tanga wapatao 200 kwa kuanzia, lakini kati ya hao 80 watapata ajira za kudumu" amesema.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.