Habari za Punde

Mkutano wa Mgombea Urais wa Zanzibar Kwa Tiketi ya CCM Uliofanyika Jimbo la Chwaka Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi akiwasili katika uwanja wa mkutano wa Kampmpira wa Chwaka akiwasalimia Wananchi wa Chwaka  baada ya kuwasili akiwa katika mikutano yake ya Kampeni kwa Wananchi wa Zanzibar kuomba Kura na kuwaombea Wagombea Wote wa Chama Cha Mapinduzi.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mhe. Balozi Seif Ali Iddi alipowasili katika jukwaa kuu la viongozi wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM uliofanyika katika viwanja vya mpira Chwaka Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwa na Viongozi wa Jukwaa Kuu wakiwa wamesimama wakati wakiimba wimbo wa Mashujaa, kabla ya kuaza kwa mkutano wa Kampeni wa CCM uliofanyika katika Uwanja wa Mpira Chwaka Wilaya ya Kati Unguja.
Baadhi ya Viongozi wakiimba wimbo wa Mashujaa wakati wa hafla ya mkutano wa Kampeni wa CCM uliofanyika katika Uwanja wa Mpira Chwaka Wilaya ya Kati Unguja. 
Baadhi ya Wanachama wa CCM Zanzibar wakishiriki katika kuimba wimbo wa mashujaa wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe.Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi, uliofanyika katika uwanja wa mpira Chwaka Wilaya ya Kati Unguja.
Vijana wa CCM wakishanilia  baada ya kumaliza kuimba wimbo wa Mashujaa wakati wa mkutano wa Kampeni ya CCM uliofanyika katika uwanja wa mpira chwaka Wilaya ya Kati Unguja.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Kati Unguja wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Mwinyi uliofanyika katika uwanja wa Mpira Chwaka na kumuombea Kura Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Mwinyi na Wabunge, Wawakilishiu na Madiwani wa CCM.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwatambulisha Wabunge na Wawakilishi wa Wilaya ya Kati Unguja wakati wa mkutano wa kampenin uliofanyika katika uwanja wa mpira Chwaka.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwatambulisha Wabunge,Wawakilishi na Madiwani wa Wilaya ya Kati Unguja wakati wa mkutano wa kampenin uliofanyika katika uwanja wa mpira Chwaka.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Mwinyi akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Kati Unguja katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mpira Chwaka Wilaya ya Kati Ungyuja na kuomba kura kwa Wananchi wa Wilaya hiyo na kuwaombea Kura Wagombea wote wa CCM. 
Mwananchi wa Wilaya ya Kati Unguja jina lake halijapatikana akimshangilia Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM wakati wa mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mpira wa Chwaka. 
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Mwinyi uliofanyika katika viwanja vya mpira Chwaka Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Mwinyi uliofanyika katika viwanja vya mpira Chwaka Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.