Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi Awaaga Watendaji wa SMZ

Maryam Mzee Yunus na Pacha wake  wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakisoma Utenzi kwenye hafla maalum ya kuagana aliyoandaliwa Balozi Seif na Uongozi wa Wizara yake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi w akizungumza na baadhi ya Watendaji na Viongozi Waandamizi wa Wizara za Serikali na Vikosi vya Ulinzi katika hafla ya kuagana rasmi iliyoandaliwa na Wizara ya Nchi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na kufanyika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {Tasaf} Nd. Ladislaus Mwamanga akitoa Tuzo Maalum kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein na Makamu wake Balozi Seif kuitokana na usimamizi mzuri kwenye Mradi wa Tasaf.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma N’hunga akitoa pongezi kabla ya kumruhusu Balozi Seif kuzungumza na baadhi ya Viongozi na Watendaji kwenye hafla ya kumuaga.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Shaaban Seif Mohamed akitoa maelezo kuhusiana na Hafla hiyo Maalum iliyoandaliwa kumuaga Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali.
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wazee, Wanawake na Waoto Mh. Modelin Cyrus Castico akitoa maelezo ya Mchango uliotolewa na Wizara yake kwa ajili ya kumtunuku Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Baadhi ya Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakijumuika pamoja kwenye hafla hiyo iliyoambatana na burdani maalum.
Baadhi ya Watejdani walio chini ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakiserebuka kwenye Taarabu Maalum ya Kikundi cha Hamasa cha Kwerekwe iliyoanikiza kwenye Hafla hiyo ya kumuaga Balozi Seif.

Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu na Wakurugenzi aliofanyakazi nao ndani ya muda wake wa Miaka Kumi ambao wengine wamestaafu na baadhi yao kuhamishwa Wizara nyengine.

Balozi Seif Kulia akimpongeza Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dr. Idriss Muslim Hijja ambae aliwahi kuwa Katibu  wa Ofisi yake kwa karibu Miaka Miwili.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mazingira Zanzibar Sheha Mjaja akimpongeza Balozi Seif kutokana na Uongozi wake uliowajengea Heshima katika Taasisi zao zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili.

Picha na – OMPR – ZNZ.


Na.Othman Khamis.OMPR.

Watumishi wachanga katika Taasisi za Umma Nchini wana wajibu wa kutekeleza majukumu yao ya kuutumikia Umma katika misingi imara ya Uzalendo itakayowawezesha kujijengea sifa na njia ya kupata fursa mbali mbali ikiwemo kupanda daraja.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akizungumza na baadhi ya Watendaji na Viongozi Waandamizi wa Wizara za Serikali na Vikosi vya Ulinzi kwa lengo la kuagana rasmi, hafla iliyoandaliwa na Wizara ya Nchi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na kufanyika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni.

Balozi Seif alisema baadhi ya Watumishi wa Kikazi kipya wamekuwa na tabia ya haraka ya Maisha kwa kutaka kubadilika ndani ya kipindi kifupi cha Utumishi wao jambo linaloweza kuwaingiza katika mabalaa kwa vile wanaweza kujikuta wakijilimbikizia Mali na fedha kinyume na Utaratibu.

“ Mtumishi wa Umma anapoanza Uwajibikaji asizingatie sifa ya kutaka kupanda cheo kwa pupa katika utendaji wake jambo ambalo ni hatari katika dhamana yake”. Alisisitiza Balozi Seif.

Balozi Seif alisema Cheo au kupanda Daraja kwa Mtumishi wa Umma ni dhamana inayokuja kufuatia umahiri na jitihada za Mtendaji husika na hili limemtia moyo kutokana na ushiriki wa Watumishi wa Wizara mbali mbali uliopelekea Taifa kujikwamua kutoka katika dimbwi la Umaskini.

Amewapongeza Viongozi na Watendaji wa Taasisi za Umma hasazile zilizo chini ya Wizara aliyoiongoza kwa kujituma Kizalendo na kupelekea mafanikio makubwa atakayoendelea kuyakumbuka katika kipindi chake chote kilichobakia cha Maisha yake.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alibainisha wazi kwamba kila wadhifa una kikomo chake kitu kilichomfanya afikie hatua ya kustaafu nyadhifa za Umma ili apate  muda wa kupumzika kama zilivyo wazi taratibu pamoja na kanuni za Utumishi wa Umma Serikalini.

Balozi Seif alisema Watumishi na Wananchi ni vyema wakaelewa kwamba hakuna Binaadamu mkamilifu hasa wale waliopewa dhamana  ya kuwahudumia Wananchi. Hivyo aliwaomba radhi wale walipopata vikwazo au usumbufu na yeye yuko moyo safi kusamehe kwa yote aliyofanyiwa.

Mapema akitoa maelezo katika hafla hiyo Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Shaaban Seif Mohamed amesema Watendaji wa Ofisi hiyo wanajivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya Uongozi wake pamoja na mwenzake Waziri wa Nchi katika kipindi chao cha Miaka Kumi.

Nd, Shaaban alisema Ofisi imefanikiwa kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia na Kibiashara baina ya Nchi na Mataifa ya Kigeni, Mashirika na Taasisi za Kimataifa na Kitaifa hali iliyotokana na ziara za Nje pamoja na Vikao na Wawakilishi wa Taasisi hizo hapa Nchini.

Alisema Uratibu mzuri wa shughuli za kukabiliana na Maafa umepelekea uelewa wa Taasisi na Wananchi juu ya hatua za kujikinga na kukabiliana na Maafa sambamba na ujenzi wa Nyumba za Waathirika wa Mvua za Masika za Mwaka 2017 Nungwi kwa Unguja na Tumbe Kisiwani Pemba.

Akimkaribisha Balozi Seif katika hadhara hiyo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma N’hunga alisema Mtendaji Mkuu huyo wa Serikali anayekaribia kumaliza muda wake ameacha Hekima na Uvumilivu katika Uongozi wake  masuala yaliyopandisha hadhi ya Uwajibikaji ndani ya Ofisi hiyo.

Mheshimiwa Mihayo alisema jambo la kupendeza lililoibuka ndani ya nyoyo ya Kiongozi huyo muadilifu ni pale aliposhinwa kusita kumuelekeza Mtendaji ye yote aliyeteleza katika utekelezaji wa majukumu yake.

Katika hafla hiyo iliyoambatana na burdani za Ngoma za Utamaduni na Taarabu ya Kisasa ilitoa nafasi kwa Viongozi Waandamizi wa Wizara za Serikali kuelezea jitihada za ujasiri wa Kiongozi huyo zilizopelekea kumtunukia zawadi mbali mbali kama ishara ya kumbu kumbu njema kwa jinsi alivyowaongoza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.