Habari za Punde

MAJALIWA APIGA KURA KIJIJINI KWAKE NANDAGALA WILAYANI RUANGWA

Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (aliyesimama mbele yake) wakiwa wamejipanga kusubiri zamu yao ya kugia katika Kituo cha Kupigia Kura cha Shule ya Msingi Nandagala wilayani Ruangwa
Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (aliyesimama mbele yake) wakiwa wamejipanga kusubiri zamu yao ya kugia katika Kituo cha Kupigia Kura cha Shule ya Msingi Nandagala wilayani Ruangwa
Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa  akipiga kura katika Kituo cha Kupigia Kura cha Shule ya Msingi ya Nandagala wilayani Ruangwa.
Mama Mary Majaliwa Mke wa Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa  akipiga kura katika Kituo cha Kupigia Kura cha Shule ya Msingi ya Nandagala wilayani Ruangwa,
Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa  akipiga kura katika Kituo cha Kupigia Kura cha Shule ya Msingi ya Nandagala wilayani Ruangwa, Oktoba 28, 2020. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amepiga kura kijijini kwake Nandagala, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.

 

Waziri Mkuu ambaye ni mbunge mteule wa jimbo la Ruangwa amepiga kura kwenye kituo cha shule ya msingi Nandagala leo asubuhi (Jumatano, Oktoba 28, 2020) akiwa na mkewe Mama Mary Majaliwa.

 

Akizungumza mara baada ya kupiga kura, Waziri Mkuu amesema zoezi la kupiga kura ni haki ya msingi na anamshukuru Mungu kwamba limeenda salama. “Ninamshukru Mungu nimeweza kushiriki haki yangu ya msingi ya kumchagua kiongozi ninayempenda ili aweze kuliongoza Taifa hili.”

 

“Kwa hapa Nandagala, Mbunge na Diwani walishapita bila kupingwa, kwa hiyo leo nimepiga kura moja tu ya kumchagua Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

 

Waziri Mkuu ambaye aliwasili kituoni saa 4:20, na kujipanga foleni yeye na mkewe, alifuata taratibu kama wananchi wengine na akaweza kupiga kura saa 4:53. Aliondoka kituoni hapo saa 5:00 asubuhi.

 

Akielezea kuhusu utaratibu mzima wa upigaji kura, Mheshimiwa Majaliwa amesema zoezi zima linaendelea vizuri na akawapongeza wasimamizi wa kituo hicho kwa sababu amekuta kuna utulivu na watu wamekaa kwenye foleni wakisubiri kuingia ndani.

 

Amesema: “Nimekuta watu wanafuata utaratibu, wanapatiwa maelekezo, vitambulisho vinahakikiwa, ni jambo la kujivunia. Amani kwetu bado ni tunu ambayo hatutakiwi kuidondosha chini ikaharibika. Ninatoa wito kwa Watanzania tujitokeze tukapige kura ili tupate viongozi wa ngazi zote ambao watatuongoza. Ni nafasi muhimu, ukiikosa leo, hutaipata tena kwa miaka mitano ijayo,” amesema.

   

IMETOLEWA:

JUMATANO, OKTOBA 28, 2020.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.