Habari za Punde

Rais Dk Hussein Ali Mwinyi kutangaza Baraza la Mawaziri kesho

 STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE

  Zanzibar                                                       18.11.2020

---

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kesho anatarajiwa kutangaza Baraza jipya la Mawaziri la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais Dk. Hussein Mwinyi anatarajiwa kutangaza Baraza hilo Ikulu Jijini Zanzibar mnamo majira ya saa nne za asubuhi ambapo matangazo ya Baraza hilo yatatangazwa moja kwa moja kupitia vyombo mbali mbali vya habari na mitandao ya kijamii ikiwemo ZBC Redio na TV, Channel Ten, Face Book ya Ikulu Habari na Youtube ya Ikulu Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Idara ya Mawasiliano na Habari Ikulu, Hassan Khatib Hassan Uteuzi wa Baraza jipya la Mawaziri unafuatia uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi uliopita, ambapo Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) alichaguliwa kushika wadhifa huo baada ya kupata asilimia 76.27 ya kura.

Kabla ya uteuzi wa Baraza jipya la Mawaziri, Dk. Hussein Ali Mwinyi tayari ameshamteua  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dk. Mwinyi Talib Haji.

Vile vile, Rais Dk. Hussein Mwinyi tayari ameshamteua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Bwana  Nahaat Mohammed Mahfoudh  pamoja na kumteua Katibu wa Rais wa Zanzibar Bwana Suleiman Ahmed Saleh.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.