Habari za Punde

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli Amemuapisha Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa Viwanja vya Ikulu Chamwino leo.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi na (kushoto kwake) Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na (kulia kwa Rais) Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano waTanzania Mhe. Job Ndugai na Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma, wakiwa wamesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa baada  ya kuwasili Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya Uapisho iliofanyika katika Viwanja vya Ikulu Chamwino leo 16/11/2020.
Waziri Mkuu Mteule Mhe. Kassim Majaliwa  akiwa na Waziri Mteule wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na  Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mteule Mhe.Profesa Palamagamba Kabudi , wakiwa wamesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla ya kuapishwa kushika nyazifa zao hizo hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma leo.
Waziri Mkuu Mteule Mhe. Kassim Majaliwa  akiwa na Waziri Mteule wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na  Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Profesa Palamagamba Kabudi , wakisubiri kuapishwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla hiyo iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma leo  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kuwa Waziri wa Fedha na Mipango katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Palamagamba Kabudi (Mb) kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharikikatika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi na (kushoto kwake) Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na (kulia kwa Rais) Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma, wakifuatilia hafla ya kuapishwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa  katika viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma leo.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika MasharikiProfesa Palamagamba Kabudi (Mb) wakila Kiapo cha Uadilifu kwa viongozi wa Umma mara baada ya kuapishwa kuwa Mawaziri na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufulikatika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 16 Novemba, 2020.

BAADHI ya Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akipiga makofi kumpongeza Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majalia baada ya kumaliza kula Kiapo katika hafla hiyo iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma leo.
Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia hafla ya kuapishwa kwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma leo 16/11/2020.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi  akizungumza na kutowa shukrani wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe, Kassim Majaliwa iliofanyika katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma leo na kushoto kwake Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wabunge wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Waziei Mkuu wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa katika viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma leo.
Viongozi wa Vyama vya Siasa Tanzania wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa  katika viwanja vya Ikulu Chamwino leo.
Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi  (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya Uapisho wa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri wa Fedha pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharikikatika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma
Viongozi wakuu wakifuatilia hutuba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kumaliza kuwaapisha Viongozi aliowateua hivi karibuni akiwemo Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, hafla hiyo ya uapisho imefanyika katika viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma leo.
Viongozi wa Dini wa Madhehebu mbambali Nchini Tanzania wakifuatilia hutuba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jogn Pombe Magufuli wakasti wa hafla ya kumuapisha Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Dodoma leo. 
Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi  (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma leo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi  akiwa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakielekea katika sehemu ilioandaliwa kwa ajili ya tafrija maalum katika viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma leo baada ya kumalizika kwa hafla ya kuapishwa Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa leo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein  Ali Mwinyi akizungumza  na kubadilisha mawazo  ( Kulia kwake ) Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa  na (kushoto kwake ) Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, wakiwa katika viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma baada ya kumalizika kwa hafla ya kuapishwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe Kassam Majaliwa leo 
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli  akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi na (kulia kwa Dk. Mwinyi ) Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na  (kushoto kwa Rais) Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakiwa katika viwanja vya IKulu Chamwino Dodoma leo baada ya kumalizika kwa hafla ya kumuapisha Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.