Habari za Punde

Zantel yarahisisha upatikanaji wa huduma kupitia duka jipya Pemba

MENEJA wa huduma kwa wateja wa Zantel, Fatma Mohammed Khalfan akizungumza na waandishi wa Habari wakati uzinduzi wa duka jipya la Zantel lilipo mjini Wete eneo la Four Ways, Kulia ni Said Masoud Ali, Meneja wa Mauzo na usambazaji Pemba, Duka hilo litarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MENEJA wa Maduka ya Zantel-Zanzibar,Mwajuma Hussein akionesha namna ya kutumia mfumo wa utoaji tiketi kwa wateja (queing System) utakaorahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja wanaotembelea duka jipya lililopo Wete-Pemba,Duka hilo litarahisisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa wakazi wa eneo hilo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MMOJA wa wateja wa Zantel, Edward Julius Kabuyu akipewa huduma katika duka jipya la Zantel lililopo mjini Wete, Pemba visiwani Zanzibar.Duka hilo litarahisisha upatikanajin wa huduma kwa wateja huku likiwa na huduma mbalimbali kukidhi mahitaji ya wateja wake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

Pemba 23, Novemba. Katika azma yake ya kuhakikisha huduma za mawasiliano zinakuwa za uhakika, Kampuni ya Zantel imezindua duka jipya ambalo litawasaidia wakazi wa kisiwa cha Pemba kupata huduma kwa urahisi zaidi.

 

Awali duka hilo lilikuwa katika eneo la Wete Sokoni na sasa limehamishiwa eneo la Pemba Four Ways ambako ni rahisi zaidi kufikika kwa wateja.

 

Duka hilo litakuwa muhimu kwa wateja wa Zantel likiwa na kituo cha huduma kwa wateja kilichoboreshwa zaidi.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo, Mkuu wa Masoko na Huduma za Kifedha wa Zantel, Sakyi Opoku alisema uwepo wa duka hilo utapunguza adha mbalimbali ambazo wateja walikumbana nazo awali.

 

“Uboreshaji wa duka hili ni sehemu ya mkakati wa kampuni yetu wa kuhakikisha tunasogeza huduma karibu na wateja ili kuhakikisha wanazipata huduma na bidhaa zetu kwa urahisi zaidi.”

 

Aliongeza “Tumehamisha duka hili kuja hapa Four Ways ukizingatia kwamba eneo hili ni rahisi kufikika si kwa wenyeji tu bali hata wageni.”

 

Duka hilo linatarajia kuhudumia zaidi ya wateja 100 likitoa huduma mbalimbali ikiwamo usajili wa simu,huduma za kifedha (Ezypesa) pamoja na uuzaji wa simu mbalimbali zenye uwezo wa 4G ikiwamo simu aina ya Smarta.

 

Duka hilo limetengenezwa kuhakikisha wateja wanapata huduma bora ikiwamo mfumo wa kidigitali wa kusajili wateja badala ya kutumia foleni ili kufanya huduma kuwa rahisi na haraka.

 

 

Kuhusu Zantel

 

Zantel ni Kampuni inyaoongoza kwa utoaji wa huduma za mawasiliano Visiwani Zanzibar kwa miaka mingi hivi sasa ikiongoza kwa ubora miundombinu ya mawasiliano, huduma pamoja na bidhaa.

 

Huduma ya kifedha ya Ezypesa ni ya kwanza nchini Tanzania kutoa huduma za kibenki za kawaida pamoja na za kiislamu kwa ushirikiano na benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

 

Aidha, Zantel ni kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za intaneti nchini Tanzania kupitia uwekezaji kwenye teknolojia ya fibre optic cable ambayo inaiunganisha Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki na duniani umeiwezesha Kampuni hiyo kuleta mapinduzi ya haraka ya kidigitali hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.