Habari za Punde

Derby ya Jang'ombe kutimua vumbi tarehe 28/12/20 Uwanja wa Amaan


Kama zilivyo 'Dabi' nyengine duniani za mpira wa miguu huisimamisha Miji, vijini na nchi, vile vile 'Dabi' hii pia huufanya mtaa wa Jang'ombe, mji, pamoja na mkoa mzima wa mjini magharibi na viunga vyake kusimama, kwani mashabiki huanza kwa kutambiana mitaa na baadae huishia uwanjani ili kuja kupokea matokeo.

Mda mwengine timu hizi zinapokutana, huwa kunahitajika nafasi ya ziada kutokana na wingi wa umati unaofika uwanjani kuburudika na mpambano huu, hivyo ulinzi huimarishwa na watazamaji wengine huwekwa katika eneo maalum la ndani ya uwanja wakiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi ili wasifike katika sehemu ya kuchezea.

NI UPI UMUHIMU WA MCHEZO HUU KWA VILABU VYOTE VIWILI?

Bila shaka kila mchezo una umuhimu katika soka. Hivyo mchezo huu pia una umuhimu mkubwa kwa vilabu vyote. 

NI UPI UMUHIMU WA TAIFA YA JANG'OMBE BOYS KATIKA MCHEZO HUU?

Ikumbukwe kwamba huu ni msimu wa pili Taifa wanapambana kurudi ligi kuu ya Zanzibar, tangu walipoteremka msimu wa 2018/19, na kwa msimu msimu huu mpya wa 2020/21 tayari Taifa wameshacheza michezo miwili na kuweka kapuni alama 4.

Hivyo Wanawania ushindi ili kuongeza alama zaidi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuduri ligi kuu ya Zanzibar.

Pia umuhimu mwengine kwa Taifa, ni kushinda na kuondoa ule uteja wa kufungwa uliozoeleka pindi timu hizi zinapokutana

Ni UPI UMUHIMU WA MCHEZO HUU KWA JANG'OMBE BOYS?

Kama ilivyo kwa Taifa ya Jang'ombe, Jang'ombe Boys na wao pia wana umuhimu mkubwa na mchezo huu.

Kwanza ni kuhakikisha wanapata matokeo chanya ya mchezo huu ili na wao kujiweka katika ramani ya kuelekea kurudi ligi kuu, ambapo wao wameshuka ligi kuu msimu wa 2019/20.

Umuhimu wa pili ni kuendeleza ubabe wa kuwafunga wapinzani wao Taifa pindi wanapokutana.

HIZI HAPA RIKODI USO KWA USO BOYS V/S TAIFA WALIZOKUTANA

Timu hizI zimeshakutana mara 10 katika historia huku mara 5 Boys akishinda, mara 3 kafungwa na mara 2 sare ambapo Dabi hiyo ya Jang’ombe kati ya Taifa ya Jang’ombe na Jang’ombe Boys ndio dabi inayoongoza kwa kuhudhuriwa na watu wengi katika uwanja wa Aman na mji mzima wa Zanzibar huwa na minong’ono mingi kabla na baada ya mchezo huo.

Msimu wa ligi wa 2017-2018 wamekutana mara mbili katika ligi kuu ya Zanzibar, ambapo Taifa walifanikiwa kuwafunga Boys magoli 2 - 1.

Na katika mchezo wa marudiano wakatoka suluhu ya 1 - 1

Msimu wa mwaka 2016-2017 walikutana Novemba 19, 2016 katika Bonanza la Coconut FM ambapo matokeo Taifa 2-0 Boys mabao ya Taifa yalifungwa na Mkongo Baraka Ushindi na Mkenya Mohd Said “Mess ambaye kwa sasa hayumo katika kikosi cha Taifa.

Disemba 10, 2016 walikutana tena kwenye Ligi kuu soka ya Zanzibar Mzunguko wa kwanza na mataokeo Taifa 2-2 Boys ambapo mabao ya Taifa siku hiyo alifunga Omar Yussuf Chande aliyetimkia klabu ya Malindi dakika 9 na Abdallah Mudhihir (Mido) ambaye amerudi kikosini kutokea Singida United dakika 60 wakati mabao ya Boys yote alifunga Khamis Mussa (Rais) dakika ya 45 na 53 ambaye ndiye Shujaa wa: Zanzibar aliyeifungia Zanzibar Heroes katika fainali ya CECAFA dhidi ya Kenya kule Machakos 2017.

Disemba 30, 2016 pia walikutana tena kwenye Kombe la Mapinduzi 2017 na matokeo Taifa 1-0 Boys kwa bao pekee lililofungwa na Hassan Seif “Banda” ambaye baadae akajiunga na Jang’ombe Boys.

Aprli 25, 2017 walikutana tena kwenye5 ligi kuu soka ya Zanzibar Mzunguko wa pili na matokeo Taifa 0-1 Boys kwa bao pekee limefungwa na Khamis Mussa “Rais” ambaye kwa sasa anaotumikia klabu ya Malindi.

Mei 14, 2017 walikutana tena kwenye ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora Mzunguko wa kwanza na matokeo Taifa 0-3 Boys ambapo mabao ya Boys yalifungwa na Khamis Mussa “Rais”, Khatib Ng’ombe alijifunga mwenyewe na Juma Mess la tatu.

Na Jumapili ya Julai 30, 2017 kwenye mzunguko wa pili ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora walikutana ambapo Boys alishinda 2-0 kwa mabao ya Hafidh Barik (Fii) aliyehamia Zimamoto kwa sasa dakika ya 6 na Juma Ali (Mess) dakika ya 66.they

8. Msimu wa Mwaka 2012-2013 Boys aliwafunga Taifa mara mbili wakati huo timu zote zipo ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini baada ya Boys kushinda 2-1 kwenye ligi hiyo, na mchezo mwengine Kombe la Waamuzi Boys tena kupata ushindi baada kushinda kwa penalti 5-4 kufuatia dakika 90 kumalizika kwa sare ya 0-0 michezo yote hiyo ilisukumwa katika Uwanja wa Mao Tsi Tung.

Wenyewe washabiki wa timu hizi huwa wana msemo wa ulio katika mfumo wa suali unaosema 'Jee tai ataruka juu, au kiwembe kitamchinja tai akishindwa kuruka?' Ingawa kwa sasa JANG'OMBE Boys wamefanya maboreshe ya nembo wamemtoa Tai katika nembo, lakini bado suali hill linaulizwa.

Mara zote majibu ya suala hilo hupatikana baada ya kumalizika dakika 90 za mchezo.

KITU KINGINE KITAKACHO NOGESHA MCHEZO HUU.

Msemaji wachachari wa Klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam Haji Manara atakuwepo katika mchezo huu, huenda akapewa fursa ya "Kick Off" sambamba na kuvikagua vilabu kabla ya Mchezo.

Njoo tarehe 28/12/2020 saa 10.00 Alasiri. Uwanjani wa Amani Zanzibar.

Kiingilio 1000 na 2000

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.