Habari za Punde

Mafunzo ya Walimu wa Takwimu wa Skuli za Serikali na binafsi yafunguliwa kituo cha Taifa cha Walimu Nkrumah


Na Maulid Yussuf WEMA


Mkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari bi Asya Iddi Issa amesema upatikanaji wa Takwimu katika masuala mbalimbali ni muhimu kwani unasidia katika kujipangia mahitaji  yanayohitajika kwa utaratibu mzuri.

Akizungumza wakati alipofungua mafunzo ya Walimu wa Takwimu wa Skuli za Serikali na binafsi Katika kituo cha Taifa cha Walimu Nkrumah, bi Asya Amesema takwimu sahihi zinasaidia katika Sehemu yeyote ikiwa Wilaya Mikoa na Taifa katika kutoa mahitaji ya msingi katika sehemu husika.

Amesema kuna baadhi ya Walimu wanekuwa na tabia ya kutoa Takwimu zisizo sahihi jambo ambalo linawatia hasara katika kufanya ufuatiliaji tena wa takwimu hizo hali ambayo inawafanya kurudi nyuma katika juhudi za kutatua matatizo yao kwa wakati.

Aidha amewataka kuwa makini katika utoaji wa taarifa sahihi ili kufanya maamuzi Na matumizi sahihi ya mahitaji ya watu au Skuli husika.

Pia amewataka kuziweka katika  kumbukumbuku wao weyewe ili kila anaehusika anapofika katika Skuli yake waweze kuzipata Pasi na usumbufu wowote.

Aidha bi Asya amewataka Walimu hao kuendelea kuwasimamia vizuri watoto katika suala zima la usafi wa mazingira pamoja na matumizi ya maji safi na salama na usafi wa mwili wanapokuwa Skuli ili kuwakinga na Maradhi mbalimbali.

Pia amewahimiza Walimu kuhakikisha wanavikagua vyoo Mara kwa mara kuanzia usafi, na ubora wake pamoja na matumizi ya maji safi na salama katika Skuli na kuwakagua Wanafunzi juu ya usafi wa mwili ili waweze kusoma wakiwa na afya njema kwa kuwakinga na maradhi mbalimbali.

Pia bi Asya amewataka walimu hasa wa Maandalizi na Msingi kujua kuwa wana dhima kubwa kwa Mungu kutokana na kuwa wao ndio walezi wakuu kwa kuwaandaa vizuri watoto katika kuwainua vizuri katika maisha yao.

Aidha bi Asya amelishukuru Shirika la UNICEF kwa msaada wanaoutoa kupitia Sekta ya Elimu ili kuhakikisha watoto wanasoma katika mazingira mazuri na salama.

Nae Msaidizi mratibu wa Mradi wa SWASH, kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, mwalimu Ame Juma Khatib amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha wanapata uelewa juu ya dhana nzima ya namna  ya kupata taarifa sahihi na zinazokwenda na wakati ili kuisaidia Serikali kupitia Wizara ya Elimu kujua mahitaji yanayohitajika katika Skuli zao na kuweza kupanga mipango yake.

Amesema Shirika la kuhudumia watoto duniani UNICEF linachukua jitihada mbalimbali kuhakikisha watoto wanasoma katika mazingira mazuri katika Skuli zote za Maandalizi, msingi na Sekondari kwa kutoa misaada mbalimbali ikiwemo mafunzo kwa Walimu pamoja na vifaaa mbalimbali vya kufundishia.

Amesema mafunzo hayo yamekuja kufuatia mradi wa usafi wa mwili, utunzaji wa mazingira pamoja na utuzaji wa vyoo (SWASH) katika Skuli ambao unalengo la kupata taarifa sahihi juu ya dhana nzima ya mradi huo.

Aidha amewataka Walimu kuwa makini katika mafunzo hayo na kuwa tayari kuyatumia kama ilivyokusudiwa, pamoja na kuishukuru Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa mashirikiano makubwa waliyoyatoa kufanikisha mafunzo hayo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.