Habari za Punde

Wafanyakazi Ofisi ya Mwansheria Mkuu wa Serikali watakiwa kuwajibika katika majukumu yao

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mzee Ali Haji akifungua mkutano wa watendaji wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na Waziri wa Nchi (OR) Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Sluleiman uliofanyika Ukumbi wa  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Mazizini Zanzibar.
Mkurugenzi Mipango uendeshaji rasilimali watu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Hamisa Mmanga Makame akisoma risala kwa niaba ya watendaji wa afisi ya Mwanasheri Mkuu katika mkutano    wa watendaji  na Waziri wa Nchi (OR) Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora uliofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Mazizini Zanzibar.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Zanzibar Mwinyi Talib Haji akimkaribisha  Waziri wa Nchi (OR) Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora  Haroun Ali Sluleiman kuzungumza na watendaji mbalimbali wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu huko Mazizini Zanzibar.

Waziri wa Nchi (OR) Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora  Haroun Ali Sluleiman akizungumza na watendaji mbalimbali wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu huko Mazizini Zanzibar.
Waziri wa Nchi (OR) Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora  Haroun Ali Sluleiman akizungumza na watendaji mbalimbali wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu huko Mazizini Zanzibar

Waziri wa Nchi (OR) Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora  Haroun Ali Sluleiman akiwa katika picha ya pamoja na  Watendaji mbali mbali  wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu huko Mazizini Zanzibar.

PICHA NA FAUZIA MUSSA/MAELEZO.

 Rahma Khamis na Rahima Mohamed Maelezo  1/12/2020

Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wametakiwa kuwajibika na kuwa wazalendo katika majukumu yao  ili kuleta ufanisi zaidi katika kazi .

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Mazizini wakati wa akimalizia ziara ya  kutembelea Taasisi zilizomo katika Wizara yake.

Amesema iwapo wafanyakazi watasimamia majukumu yao kwa uadilifu na uwajibikaji wataweza kufikia lengo na kuondoa malalamiko yanayoweza kujitokeza katika utendaji wa kazi kwa kuzingatia sheria,taratibu na kanuni za kazi.

Amesema kuwa Zanzibar itajengwa na Wazanzibari wenyewe kwa kuthamini kazi walizopewa hivyo kuna wajibu wa kila mfanyakazi kuheshimu sheria na kanuni za uwajibikaji ili kufikia lengo la Rais kwa kutaka kuinyanyua Zanzibar kiuchumi.

“Zanzibar tuhakikishe tunaitetea na kuijenga kwa nguvu zetu zote hivyo kila mmoja awajibike katika eneo lake kazi alilopangiwa na afike na kuondoka kwa wakati ulioweka na sheria za utumishi” alisema Waziri.

Aidha amewahakikishia wafanyakazi hao kuwa atasimamia ipasavyo kuhakikisha wanapata nafasi ya kutosha kwa kuongeza ghorofa mbili na kwa upande wa Pemba watajenga jengo la Ofisi yenye nafasi ya kutosha hivyo amewataka waandae michoro kwa ajili ya ujenzi huo.

Sambamba na hayo Waziri huyo amemtaka mwanasheria Mkuu kuendelea kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa wafanyakazi wake ili kuwaongezea ujuzi zaidi ili  kuleta ufanisi katika kazi .

Nae Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dkt Mwinyi Talib Haji ameahidi kusimamia maslahi ya wafanyakazi wake na kuwaendeleza kimasomo ili kuondoa malalamiko kwa baadhi ya wafanyakazi hao.

Aidha amesema Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ina rasilimali watu wa kutosha hivyo kwa umoja wao watajitahidi kuyatekeleza yale ambayo yanategemewa kisheria na kikatiba ili kufikia malengo  yaliyokusudiwa.     

Akitoa taarifa fupi Mkurugenzi Mipango Uendeshaji Rasilimali watu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Hamisa Mmanga Makame amesema kuwa Ofisi inahitaji  Wakili dhamana ambae atakuwa Msimamizi Mkuu wa Ofisi kwa upande wa Pemba.

Amesema kuwa katika kutekeleza majukumu yake idara imeshughulikia na kuandaa kanuni 13 zinazotokana na sheria tofauti kwa lengo la kuzifanya sheria hizo ziweze kutekelezeka kwa ufanisi zaidi.

Aidha amefahamisha kuwa kesi 46 zimesimamiwa kwa kipindi cha Julai hadi Septemba kati ya kesi hizo tayari kesi tano zimeshatolewa hukumu, na  kesi 41 zinaendelea ambapo kwa Unguja kesi 34 zimesimamiwa na kwa upande wa Pemba kesi 7 zimesimamiwa

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.