Habari za Punde

Naibu Waziri Mifugo Atembelea Kiwanda Cha Tanchoice

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, Wakala ya Maabara ya Veterinari (TVLA), Dkt. Stella Bitanyi akimuonesha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul moja ya chanjo wanazozalisha alipotembelea Kituo cha Wakala hiyo cha kutengeneza chanjo kilichopo Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani 

Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha TANCHOICE, Selo Luwongo (wa pili kutoka kushoto) akimuonesha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (wa pili kulia) maroli yaliyopakiwa minofu ya nyama ya mbuzi zaidi ya Tani 40 kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi alipotembelea Kiwanda hicho Januari 11, 2021. Kulia ni Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama, Imani Sichwale.

Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha TANCHOICE, Selo Luwongo (kushoto) akimuonesha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (wa tatu kutoka kushoto) mbuzi waliochinjwa na kuhifadhiwa katika chumba chenye baridi kali kwa ajili ya kusafirishwa kuuzwa nje ya nchi. Gekul alitembelea kiwanda hicho kilichopo Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani 
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, Wakala ya Maabara ya Veterinari (TVLA), Dkt. Stella Bitanyi (kulia) akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (katikati) alipotembelea Kituo cha Wakala hiyo kilichopo Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani Januari 11, 2021. Kushoto ni Kaimu Msajili, Bodi ya Nyama, Imani Sichwale.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.