Habari za Punde

Rais Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar pamoja na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Chato mkoani Geita

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad mara baada ya kuzungumza na Wanahabari katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 14 Januari 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad mara baada ya mazungumzo yao katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 14 Januari 2021.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad akizungumza na Wanahabari mara baada ya kikao chao cha pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari mara baada ya mazungumzo yao ya pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.