Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Mhe.Dk Hussein Ali Mwinyi Mgeni rasmin Fainali ya Mapinduzi Cup Kati ya Simba na Yanga Mchezo Uliofanyika Jana Usiku Uwanja wa Amaan.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Yanga kabla ya kuaza mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi Cup mchezo uliofanyika jana katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar Timu ya Yanga imeibuka Bingwa wa Mapinduzi Cup 2021 -2022.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Timu ya Simba kabla ya kuaza kwa mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi Uliofanyika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi alikuwa mgeni rasmin katika fainali za mashindano ya Kombe la Mapinduzi ambapo Yanga SC ilitawazwa kuwa bingwa wa mashindano hayo kwa mwaka huu 2021.

Mashindano hayo ni miongoni mwa shamrashamra za sherehe za miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Timu ya Yanga SC wamefanikiwa kutwaa Kombe hilo la Mapinduzi Cup baada ya ushindi wa penenti 4-3 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 za mchezo huo uliofanyika  usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa Amaan, Jijini Zanzibar.

Shujaa wa Yanga SC kwenye mchezo huo ambao mgeni rasmin alikuwa Rais Dk. Mwinyi alikuwa ni kipa Farouk Shikaro aliyeokoa penanti  ya mwisho ya Simba iliyopigwa na Mkenya mwenzake beki Joash Onyango.

Penalti za Yanga SC zimefungwa na MkongoTuisila Kisinda, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Zawadi Mauya na Mrundi Said Ntibanzokiza wakati Mkongo mwingine MukokoTonombe iliokolewa na kipa Beno Kakolanya wa Simba.

Penalti za Simba SC zilifungwa na kiungo Mkenya Francis Kahata, mshambuliaji Mkongo Chriss Mugalu na beki mzawa Gardiel Michael, wakati mshambuliaji Mnyarwanda, Meddie Kagere na Nanodhawa Dabihiyo aligongesha mwamba wa juu wa goli kulia.

Hiyo itakuwa ni mara ya pili Yanga SC kutwaa Kombe la Mapinduzi baada ya mwaka 2007 mashindano hayo yalipofanyika kwa mara ya kwanza ambapo waliifunga Mtibwa Sugar kwenye fainali.

Nyota watatu wa Simba walijinyakulia tuzo baada ya mchezo huo, Wakenya beki Joash Onyango Mchezaji Bora wa Mechi, Kiungo Francis Kahata Mchezaji Bora wa Mashindano hayo ni Mshambuliaji Miraj Athumani Mfungaji Bora kwa mabao yake manne, Mkenya mwingine kipa Farouk Shikaro wa Yanga amejinyakulia tuzo ya Kipa Bora kufuatia kuruhusu bao moja tu kwenye mashindano hayo.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Farouk Shikhalo, Kibwana Shomari, Adeyoum Saleh/Paul Godfrey ‘Boxer’ dk71, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Said Juma ‘Makapu’, MukokoTonombe, Tuisila Kisinda, Zawadi Mauya, Michael Sarpong/Waziri Junior dk8, Said Ntibanzokizana Haruna Niyonzima.

Simba SC; Beno Kakolanya, David Kameta, Gardiel Kameta, Kennedy Juma, JoashOnyango, ThadeoLwanga, Hassan Dilunga/Chris Mugalu dk61, MuzamilYassin, MeddieKagere, Francis KahatanaMirajJuma/Ibrahim Ajibu dk72.

ViongozimbalimbaliwavyamavyasiasanaSerikaliyaMapinduziya Zanzibar naSerikaliyaJamhuriyaMuunganowa Tanzania walihudhuriakatikamtanangehuoambapomaelfuyamashabikiwalihudhurianakujazauwanjanawenginekadhaakusalianjeyauwanja.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.