RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha akiongozana na Ujumbe wake na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA Bw. Makame Kh. Hassan (kushoto kwake) mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo (kushoto kwa Rais) akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha na (kulia kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Kitabu cha Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji wa Awamu ya Tatu 2017/2022 akikabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo, baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika Ikulu kujitambulisha hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo, baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo 25-2-2021.(Picha na Ikulu)
STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar
25.02.2021
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Hussein Ali Mwinyi amepongeza mashirikiano makubwa yanayotolewa na Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) kwa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi
Zanzibar (ZAECA).
Rais Dk. Mwinyi
aliyasema hayo leo Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU)
Brigedia Jenerali John Mbungo akiwa amefuatana na ujumbe wake.
Katika mazungumzo hayo,
Rais Dk. Mwinyi alisisitiza haja ya kuendelezwa kwa mashirikiano hayo hasa
ikizingatiwa kwamba (TAKUKURU) ni Taasisi ya siku nyingi na ina uzoefu mkubwa.
Alieleza kuwa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar ina azma ya kuijengea uwezo hivyo, katika masuala ya
uchunguzi, mafunzo na shughuli zote zinazofanywa na (TAKUKURU) basi watajifunza
kutoka Taasisi hiyo.
“Tunashukuru kwa
milango yenu kuwa wazi na tutaomba kuendelea kwa sababu tunataka kukifanya
chombo hichi kuwa imara zaidi na hatuna sehemu nyengine ya kupata uzoefu kama si TAKUKURU ”, alisisitiza Rais
Dk. Mwinyi.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi
alieleza haja ya kuwa na muundo kama ule wa (TAKUKURU) ikiwa ni pamoja na
kushuka katika ngazi za Mikoa na Wilaya licha ya hali hiyo kuhitaji uwezo
mkubwa lakini ni vyema wakaanza ili kazi wanazozifanya ziwe rahisi zaidi badala
ya kutegemea ngazi za makao makuu pekee.
Alisema kuwa ni vyema (ZAECA)
ikajifunza kutoka Taasisi ya (TAKUKURU) kutokana na mambo mbali mbali ya
kuiendesha Taasisi hiyo.
Alitoa shukurani kwa
Taasisi ya (TAKUKURU) kwa kuonesha utayari wao wa kuwasaidisa ZAECA, na
kusisitiza kwamba katika wakati huu uliopo Taasisi hiyo ina umuhimu wa pekee
kwani uzoefu unaonesha duniani kwamba katika kuhakikisha rushwa inadhibitiwa ni
lazima kuwepo kwa chombo cha kusimamia uadilifu.
Nae Brigedia Jenerali John Mbungo, Mkurugenzi Mkuu
wa (TAKUKURU) huyo aliyeteuliwa mwaka jana Mei 2020, ambaye mwanzo alikuwa
Naibu Mkurugrnzi Mkuu alisema kuwa ujio wake ni kwa ajili ya kujitambulisha
pamoja na kuwatembelea washirika wenzao (ZAECA).
Alisema kuwa (TAKUKURU)
imekuwa ikishirikiana vyema na (ZAECA) katika mambo mali mbali ikiwa ni pamoja
na kushirikiana katika mafunzo ya weledi hasa ikizingatiwa kwamba (TAKUKURU)
ina uzoefu mkubwa kutokana na kutangulia kuanzishwa kwani Taasisi hiyo imeanzishwa
mwaka 1975 ambapo (ZAECA) imeanzishwa mwaka 2013.
Alisema kwamba (TAKUKURU)
ni Taasisi ya kwanza kuanzishwa katika bara la Afrika, hivyo ina uzoefu mkubwa katika
kuendesha shughuli zake.
Pamoja na hayo,
Bregedia Jenerali Mbugo alisema kuwa Taasisi hizo mbili zimekuwa zikishiriki vyema
katika vikao mbali mbali vya Kimataifa kwa pamoja na kuangalia vipi Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inaweza kunufaika na vikao hivyo.
Alisema kuwa wamekuwa
wakikaa pamoja na kujadili mambo kadhaa kuhusu vikao hivyo ambapo pia, kwa vile
wote ni wanachama wa Mkataba Mkuu wa Kimataifa wa Mapambano dhidi ya Rushwa,
hivyo wamekuwa wakihudhuria pamoja vikao hivyo na kuangalia vipi nchi inaweza
kunufaika sambamba na kuhudhuria vikao vya Afrika Mashariki ambapo pia ina
sehemu ya masuala ya rushwa.
Aidha, alieleza namna
wanavyoshiriki pamoja vikao vya nchi za Kusini mwa Afrika ambavyo hukaa pamoja
mara baada ya kumaliza vikao hivyo na kujadili kwa pamoja namna ya utekelezaji
wa masuala hayo.
Wakati huo huo, Rais Dk. Mwinyi
alikutana na uongozi wa Jumuiya ya Wazee Zanzibar (JUWAZA) katika ukumbi wa
Ikulu Jijini Zanzibar na kuipongeza Jumuiya hiyo kwa ushirikiano wanaotoa kwa
Serikali.
Katika mazungumzo
hayo, Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa Jumuiya hizo zinahitajika kutokana na umhimu
wake mkubwa ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wake kwa Serikali kwani si mambo
yote Serikali inaweza kuyafanya.
Rais Dk. Mwinyi
alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na
Jumuiya hizo kwa azma ya kuhakikisha wazee nao wananufaika.
Sambamba na hayo, Rais
Dk. Mwinyi alieleza mafanikio makubwa yatakayopatikana kutokana na vitambulisho
vinavyotolewa kwa ajili ya wazee.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi
alitoa pongezi kwa Naibu Katibu Mkuu Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto
Abeida Rashid Abdallah kwa ushirikiano wake mzuri anaouonesha kwa Jumuiya hizo
na kumtaka kuendelea.
Mapeuongozi wa Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment