Habari za Punde

Wajumbe watano wa chama cha ACT Wazalendo waapishwa leo na Spika Baraza la Wawakilishi

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akumuapisha  Mwakilishi wa kuteuliwa  wa Chama cha ACT-Wazalendo Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika leo katika ukumbi wa mkutano wa Baraza Chukwani Jijini Zanzibar. 
Baadhi ya viongozi waandamizi wa ACT waliofika Baraza la Wawakilishi leo kushuhuduia kuapishwa kwa wajumbe watano kutoka chama cha ACT Wazalendo
Mwakilishi wa kuteuliwa kutoka katika chama cha ACT Wazalendo, Mh Omar Said Shaaban akila kiapo mbele ya Spika wa Baraza la Wawakilishi mhe Zubeir Ali Maulid
 

Mkutano wa pili wa Baraza la 10 la Wakilishi unaoendelea Chukwani Mjini Zanzibar umeanza kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, kuwaapisha wajumbe watano wa chama cha ACT Wazalendo baada ya chama hicho kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa.


Wajumbe hao ni Habib Ali Mohammed kutoka Jimbo Mtambwe, Hassan Omar Hamad kutoka jimbo la Kojani na Kombo Mwinyi Shehe kutoka Jimbo la Wingi walichaguliwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita, wengine ni Nassor Ahmed Mazrui na Omar Said Shaaban Walioteliwa na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.