Habari za Punde

Kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia huleta changamoto kwa akinamama 

Na Muhammed Khamis,TAMWA-Z’bar.

 

Afisa uwezeshaji uchumi wanawake kupitia mradi wa Viungo Zanzibar Nairat Abdalla Ali amesema kukosekana kwa usawa wa kijinsia katika jamii wanawake wengi wakiwemo watu wenye ulemavu  wataendelea kukabiliwa na changamoto mbali mbali zikiwemo za umiliki wa ardhi pamoja na kutokukua kiuchumi.

 

 Afisa huyo aliyasema hayo alipokua akizungumza na waandishi  habari mjini Unguja wakati walipokua wakitoa mafunzo kwa wakulima mbali mbali nkutoka wilaya yatatu za Unguja ambazo ni Wilaya ya kusini,Magharib A pamoja na Wilaya ya kati.

 

Alisema wanawake wengi Zanzibar wamekua wakikosa haki za msingi kutokana na uwepo wa vizingiti tofauti vikiwemo vya baadhi ya wanaume kuwawekea vikwanzo wanawake wakidhani kuwa si watu wanaohitaji kupatiwa fursa muhimu jambo ambalo linaendelea kurudisha nyuma jitihada za wanawake.

 

Alieleza kuwa kwa kuliona hilo kupitia mradi huo wa viungo wameona ipo haja kutoa elimu ya jinsia kwa wakulima hao na wengine wengi ambao wanaamini elimu hio itakwenda kubadili mtazamo na hatimae wanawake wengi kupewa fursa zikiwemo za umiliki ea ardhi na hata kushiriki uuzaji wa bidhaa zao masokoni.

 

‘’Tunaamini kuwa elimu hii itawazindua wanaume hawa na wanawake walioshoriki na watakaoendelea kushiriki hatimae kubapata mabadiliko makubwa’’aliongezea.

 

Sambamba na hayo Afisa huyo alisema ili jamii yoyote hile iweze kupiga hatua zaidi kimaendelea hakuna budi kuwepo kwa usawa wa kijinsia bila ya ubaguzi wa haki kwa wanaume na wanawake.

 

Kwa upande wake mtaalamu wa maswala ya kijinsia kutoka wizara ya afya Zanzibar Halima Abdulrahman Omar alisema bado kwenye jamii kuna matatizo mbali mbali ambayo yakiendelea kunyamaziwa hayataweza kuondoka.

 

Alisema matatizo hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na jamii wenyewe yamekua na athari kubwa kwa wanawake wengi hususani vijijini kukosa haki zao za msingi ambazo wangepaswa kuzipata kama wanaume.

 

Alieleza kuwa wanawake wengi hivi sasa si watu wenye kumiliki mambo muhimu kama bile ardhi na nyumba badala yake wameaki kusubiri kutoka kwa waume zao na ndio maana ndoa nyingi zinapovunjia wahanga hubaki kuwa wanawake.

 

Sambamba na hilo alisema kuwepo kwa mazingira hayo kunatokana na malezi kwa baadhi ya familia ambayo huamini kuwa watoto wa kiume ndio hupaswa kufanya shughuli zote zinazotumia nguvu na kusoma zaidi huku wanawake wakibaki kufanya kazi za nyumbani.

 

‘’Kwa mtazamo huu ndio maana hadi leo hii wanawake wengi wanaedelea kuamini kuwa wao hawapaswa kumili ardhi wala kuwa na majumba bali wanapaswa kubaki kuwa mama wa nyumbani tu’’aliongezea.


Pamoja na hayo aliwataka wanawake nkubadili mtazamo na kuacha kufikiri zaidi kwenye kuwekeza mapambo ikiwemo vitu vyya dhahabu na nguo badala yake wanapaswa pia kufikiri kwenye suala zila la umiki wa ardhi na nyumba pia kujikita kwenye kilimo.

 

Badhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema elimu waliopata kupitia mradi wa viungo imekuja wakati sahihi ukizingatia kuwa watahakikisha wanatoa fursa kwa wake zao na wanawake wengine kwenye jamii kufanya shughuli zan kilimo pasi na kuwawekea vikwazo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.